Langkau ke kandungan
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Maaida
Surah 5

Al-Maaida

Ini ialah terjemahan Tafsir as-Saʿdī seperti yang diterbitkan oleh IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca daripada halaman-halaman laman itu. Laman itu tidak menyatakan siapa yang menterjemahkannya atau edisi cetakan mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan syarat untuk mengambil teksnya, maka hak untuk memaparkannya belum disahkan. Belum ada sesiapa yang membandingkannya dengan buku bercetak, dan tiada ulama yang menyemaknya. Setiap bahagian berada di sisi ayat-ayat yang diulasnya, iaitu teks Al-Quran daripada Tanzil, dipaparkan seperti yang ada di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh laman itu berada bersama bahagian sebelumnya, dan indeks menamakan setiap ayat sedemikian. Sabīl tidak menulis atau menterjemahkan satu pun daripadanya.

Teks daripadasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil pada 2026-10-22

Ayat 108

ذَٰلِكَ أَدْنَىٰٓ أَن يَأْتُوا۟ بِٱلشَّهَـٰدَةِ عَلَىٰ وَجْهِهَآ أَوْ يَخَافُوٓا۟ أَن تُرَدَّ أَيْمَـٰنٌۢ بَعْدَ أَيْمَـٰنِهِمْ ۗ وَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ وَٱسْمَعُوا۟ ۗ وَٱللَّهُ لَا يَهْدِى ٱلْقَوْمَ ٱلْفَـٰسِقِينَ 108

{108} Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema katika kueleza hekima ya ushahidi huo, na kuusisitiza, na kuurudisha kwa wasimamizi wa maiti inapodhihirika hiana kutoka kwa hao mashahidi wawili. "Hivyo ni karibu zaidi kwamba watatoa ushahidi ulio sawa" pindi vinaposisitizwa juu yao hivyo visisitizo. “Au wataogopa visije vikaletwa viapo vingine baada ya viapo vyao." Yaani, visikubaliwe viapo vyao, kisha virudishwe kwa wasimamizi wa maiti; "Na Mwenyezi Mungu hawaongoi kaumu ivukayo mipaka;" yaani, wale sifa yao ni kuvuka mipaka, wala hawataki uwongofu na kuielekea njia iliyonyooka. Na jumla ya haya ni kwamba mauti yanapomfikia maiti katika safari au mfano wake miongoni mwa penye uwezekano mkubwa wa uchache wa mashahidi wa kuaminika, kwamba inampasa awausie mashahidi wawili Waislamu, waadilifu. Na asipopata isipokuwa mashahidi wawili makafiri, basi inaruhusika awausie. Lakini kwa sababu ya ukafiri wao, ikiwa wasimamizi wa maiti watawatilia shaka, basi watawapisha baada ya Swala kwamba hawakuhaini, wala hawakusema uongo, wala hawakugeuza, wala hawakubadilisha chochote, na kwa hilo wanakuwa hawana hatia katika haki iliyoelekezwa kwao. Na ikiwa hawatawaamini, na wakapata ushahidi kwamba mashahidi hao wawili ni waongo, basi ikiwa wasimamizi wa maiti wanataka, basi na wawasimamishe wawili kati yao na waape kwa Mwenyezi Mungu kwamba ushahidi wao unastahiki zaidi kuliko ushahidi wa mashahidi wale wawili wa mwanzo, na kwamba wao walifanya hiana na kusema uongo, kwa hiyo wanastahiki zaidi kile wanachodai kuwaliko wao. Na Aya hizi tukufu ziliteremshwa kuhusiana na kisa maarufu cha Tamim ad-Dari na 'Adi bin Bad-a, pale Al-'Adawi alipowausia. Na Mwenyezi Mungu ndiye anayejua zaidi. Na Aya hizi tukufu zinatumika kama ushahidi juu ya hukumu kadhaa: Miongoni mwake ni kwamba, wasia uko katika sheria, na kwamba mtu ambaye yuko karibu kufa anafaa kuusia. Na miongoni mwake ni kwamba, unazingatiwa hata kama mtu huyo amefikia mwanzo na dalili za kifo, maadamu akili yake imetulia. Na miongoni mwake ni kwamba, ushahidi juu ya Wosia ni lazima uwe kwa watu wawili waadilifu. Na miongoni mwake ni kwamba, ushahidi wa makafiri katika jambo hili na mfano wake unakubalika kwa sababu ya kuwepo kwa dharura. Na hili ndilo dhehebu la Imam Ahmad. Na wengi miongoni mwa wanachuoni walidai kuwa hukumu hii ilibatilishwa, lakini haya ni madai ambayo hayana ushahidi. Na miongoni mwake ni kwamba, inaweza kunufaika kutokana na ishara na maana ya hukumu, kwamba ushahidi wa makafiri wakati hakuna mtu mwingine yeyote. Hata katika mambo mengine yasiyokuwa suala hili, unakubalika, kama Sheikh al-Islam Ibn Taymiyyah pia alikuwa na maoni haya. Na miongoni mwake ni muislamu kuruhusika kusafiri pamoja na kafiri ikiwa hakuna lililokatazwa. Na miongoni mwake ni kuruhusika kusafiri kwa ajili ya biashara. Na miongoni mwake ni kwamba, mashahidi wawili hao ikiwa kutakuwa na shaka juu yao, na kusiwepo na ushahidi unaoonyesha hiana yao, na wasimamizi wanataka kusisitiza hayo juu yao kwa kiapo, na kuwazuia baada ya swala, kisha waape kwa namna aliyoitaja Mwenyezi Mungu. Na miongoni mwake ni kwamba, hakutakuwa na tuhuma wala shaka, basi hakutakuwapo na haja ya kuwazuilia na kusisitiza kiapo juu yao. Na miongoni mwake ni kutukuza jambo la kutoa ushahidi, kwa kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu aliufungamanisha na nafsi yake; na kwamba ni lazima kuutunza na kuutekeleza kwa uadilifu. Na miongoni mwake ni kwamba, inaruhusika kuwapa mtihani mashahidi wawili hao wakati kuna shaka juu yao na kuwatenganisha ili kuuchunguza ushahidi wao. Na miongoni mwake ni kwamba ikiwa kuna dalili inayoonyesha kwamba wawili wale waliousiwa katika suala hili walisema uongo; basi wasimamizi wawili wa maiti watasimama na waape kwa Mwenyezi Mungu kwamba; "viapo vyetu ni vya kweli zaidi kuliko vyao, na walifanya hiana na kusema uongo." Kisha watapewa yale waliyodai, na unakuwa ushahidi huo pamoja na viapo vyao wenye kusimama pahali pa uthibitisho.