Langkau ke kandungan
Tafsir As-Saadi - Swahili · An-Nisaa
Surah 4

An-Nisaa

Ini ialah terjemahan Tafsir as-Saʿdī seperti yang diterbitkan oleh IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca daripada halaman-halaman laman itu. Laman itu tidak menyatakan siapa yang menterjemahkannya atau edisi cetakan mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan syarat untuk mengambil teksnya, maka hak untuk memaparkannya belum disahkan. Belum ada sesiapa yang membandingkannya dengan buku bercetak, dan tiada ulama yang menyemaknya. Setiap bahagian berada di sisi ayat-ayat yang diulasnya, iaitu teks Al-Quran daripada Tanzil, dipaparkan seperti yang ada di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh laman itu berada bersama bahagian sebelumnya, dan indeks menamakan setiap ayat sedemikian. Sabīl tidak menulis atau menterjemahkan satu pun daripadanya.

Teks daripadasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil pada 2026-10-22

Ayat 17–18

إِنَّمَا ٱلتَّوْبَةُ عَلَى ٱللَّهِ لِلَّذِينَ يَعْمَلُونَ ٱلسُّوٓءَ بِجَهَـٰلَةٍ ثُمَّ يَتُوبُونَ مِن قَرِيبٍ فَأُو۟لَـٰٓئِكَ يَتُوبُ ٱللَّهُ عَلَيْهِمْ ۗ وَكَانَ ٱللَّهُ عَلِيمًا حَكِيمًا 17 وَلَيْسَتِ ٱلتَّوْبَةُ لِلَّذِينَ يَعْمَلُونَ ٱلسَّيِّـَٔاتِ حَتَّىٰٓ إِذَا حَضَرَ أَحَدَهُمُ ٱلْمَوْتُ قَالَ إِنِّى تُبْتُ ٱلْـَٔـٰنَ وَلَا ٱلَّذِينَ يَمُوتُونَ وَهُمْ كُفَّارٌ ۚ أُو۟لَـٰٓئِكَ أَعْتَدْنَا لَهُمْ عَذَابًا أَلِيمًا 18

{17-18} Kukubali toba ambako kuko juu ya Mwenyezi Mungu kutoka kwa waja wake ni kwa aina mbili: Kumwezesha kwake kutubia, na kuikubali baada ya kupatikana kwake kutoka kwa mja. Kwa hivyo, akajulisha hapa kwamba toba inayostahiki juu ya Mwenyezi Mungu kama haki aliyoiweka mwenyewe juu ya nafsi yake, kutokana na ukarimu kutoka kwake na kutoa kwake kwa wingi kwa aliyefanya ubaya, yani maasia "kwa kutojua." Yani, kwa kutojua kwake matokeo yake, na kuleta kwake ghadhabu ya Mwenyezi Mungu na adhabu yake, na kutojua kwake kwamba Mwenyezi Mungu anamtazama na kumchunga, na kutojua kwake mwisho wake miongoni mwake kupunguza imani au hata kuiondoa imani. Basi kila mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu ni mjinga wa kuzingatia haya hata kama anajua uharamu wake. Bali kujua uharamu wake ni sharti kwa kuwa ni dhambi inayoadhibiwa. "Kisha wakatubia kwa haraka," inawezekana maana yake ikawa: Kisha wakatubu kabla ya kushuhudia mauti. Kwa maana, bila ya shaka Mwenyezi Mungu huikubali toba ya mja ikiwa atatubia kabla ya kushuhudia mauti na adhabu. Na ama baada ya kuja kwa mauti, basi haikubaliwi toba kutoka kwa muasi, wala kurudi kutoka kwa makafiri. Kama alivyosema Yeye Mtukufu kuhusu Firauni, "Mpaka alipofikiwa na kuzama, akasema: Nimeamini kuwa hapana mungu isipokuwa yule ambaye walimwamini Wana wa Israili, na mimi ni miongoni mwa Waislamu!" hadi mwisho wa Aya. Na akasema Yeye Mtukufu, "Walipoiona adhabu yetu, walisema: Tumemwamini Mwenyezi Mungu peke yake, na tunaikufuru miungu tuliyokuwa tukiishirikisha naye. Lakini imani yao haikuwa yenye kuwafaa kitu wakati ambao wamekwisha iona adhabu yetu. Huu ndio mwendo wa Mwenyezi Mungu ambao ulikwishapita kwa waja wake." Na akasema hapa, "Wala hawana toba wale wafanyao maovu mpaka yakamfikia mmoja wao mauti, kisha hapo akasema: Hakika, mimi sasa nimetubia. Wala wale wanaokufa hali ya kuwa wao ni makafiri. Hao tumewaandalia adhabu chungu." Na hilo ni kwa sababu toba katika hali hii ni toba ya kulazimika ambayo haimnufaishi mwenyewe. Lakini toba ya hiari ndiyo inayofaa. Inawezekana kuwa maana ya kauli yake, "kisha wakatubia kwa haraka" kuwa ni karibu na kitendo chao cha dhambi inayolazimu kutubia. Kwa hivyo, maana ni kwamba yeyote anayeharakisha kuacha tangu dhambi ilipotolewa na akarudi kwa Mwenyezi Mungu na akajuta juu yake, basi Mwenyezi Mungu anamkubalia toba yake. Tofauti na yule anayeendelea katika dhambi yake - na akasisitiza juu ya aibu zake mpaka zikawa ni sifa thabiti ndani yake, basi ni vigumu kwake kupata toba kamili. Na kuna uwezekano mkubwa kwamba hatawezeshwa kutubia wala hatarahisishiwa sababu zake. Kama yule atendaye maovu kwa elimu iliyomfikia na yakini, na akipuuza kutazama kwa Mwenyezi Mungu juu yake, basi yeye anajifungia mlango wa rehema. Ndiyo, Mwenyezi Mungu anaweza kumwezesha mja wake ambaye anadumu katika dhambi kwa kukusudia na kwa yakini, na akatubia toba yenye manufaa ambayo kwayo anafuta mabaya yake yaliyopita na makosa yake yaliyopita. Lakini rehema na kuwezeshwa kwa yule wa kwanza iko karibu zaidi. Na kwa sababu ya hili, akahitimisha Aya ya kwanza kwa kauli yake, "Na Mwenyezi Mungu ni mwenye kujua, Mwenye hekima." Na katika kujua kwake ni kwamba anajua toba ya kweli na ya uongo. Kwa hivyo, anamlipa kila mmoja wao kulingana na anavyostahiki kwa hekima yake. Na katika hekima yake ni kumwezesha yule ambaye hekima yake na rehema yake inataka awezeshwe kutubia, na anampuuzilia mbali yule ambaye hekima yake na udilifu wake unataka asiwezeshwe. Na Mwenyezi Mungu ndiye anayejua zaidi.