Langkau ke kandungan
Tafsir As-Saadi - Swahili · An-Nisaa
Surah 4

An-Nisaa

Ini ialah terjemahan Tafsir as-Saʿdī seperti yang diterbitkan oleh IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca daripada halaman-halaman laman itu. Laman itu tidak menyatakan siapa yang menterjemahkannya atau edisi cetakan mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan syarat untuk mengambil teksnya, maka hak untuk memaparkannya belum disahkan. Belum ada sesiapa yang membandingkannya dengan buku bercetak, dan tiada ulama yang menyemaknya. Setiap bahagian berada di sisi ayat-ayat yang diulasnya, iaitu teks Al-Quran daripada Tanzil, dipaparkan seperti yang ada di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh laman itu berada bersama bahagian sebelumnya, dan indeks menamakan setiap ayat sedemikian. Sabīl tidak menulis atau menterjemahkan satu pun daripadanya.

Teks daripadasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil pada 2026-10-22

Ayat 114

لَّا خَيْرَ فِى كَثِيرٍ مِّن نَّجْوَىٰهُمْ إِلَّا مَنْ أَمَرَ بِصَدَقَةٍ أَوْ مَعْرُوفٍ أَوْ إِصْلَـٰحٍۭ بَيْنَ ٱلنَّاسِ ۚ وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ ٱبْتِغَآءَ مَرْضَاتِ ٱللَّهِ فَسَوْفَ نُؤْتِيهِ أَجْرًا عَظِيمًا 114

{114} Yani hakuna heri yoyote katika mengi ya wanayozungumza watu kwa siri na kuongeleshana. Na ikiwa hakuna heri ndani yake, basi ima hakuna manufaa ndani yake; kama vile maneno bure yanayoruhusiwa, au ni uovu yenye madhara matupu; kama vile maneno ya haramu kwa aina zake zote. Kisha Yeye Mtukufu akatoa katika hilo, akasema, "Isipokuwa kwa yule anayeamrisha kutoa sadaka." Kama vile mali, au elimu, au manufaa yoyote yale, bali hata ibada zinazofungamana na mtu mwenyewe huenda zikaingia humo. Kama vile kufanya tasbihi (kumtakasa Mwenyezi Mungu), na kumhimidi Mwenyezi Mungu na kadhalika. Kama alivyosema Nabii -rehema na amani zimshukie, “Hakika kwa kila tasbihi kuna sadaka, na kwa kila takbira kuna sadaka, na kwa kila tahlil kuna sadaka, na kuamrisha mema ni sadaka, na kukataza maovu ni sadaka, na kujamiana kwa mmoja wenu kuna sadaka...” hadi mwisho wa hadithi. "Au kutenda mema." Nayo ni wema, na utii, na kila kitu kinachojulikana katika sheria na akili kwamba ni kizuri. Na kuamrisha mema kunapotajwa bila ya kuunganishwa na kukataza maovu, kukataza maovu kunaingia humo. Hilo ni kwa sababu kuacha yale yaliyoharamishwa ni katika mema. Na pia haitimii kufanya mema isipokuwa kwa kuacha maovu. Na ama mawili haya yanapounganishwa, basi wema unaelezwa kwa kufanya yale yaliyoamrishwa, nayo maovu kwa kuyaacha yaliyokatazwa. "Au kupatanisha baina ya watu:" Na upatanisho haiwi isipokuwa kati ya wale wanaozozana, wenye mgogoro. Na kuzozana na kugombana na kukasirikiana husababisha uovu na mgawanyiko ambao hauwezi kuwekewa mipaka. Kwa hivyo, sheria ilihimiza juu ya upatanisho kati ya watu katika damu, na mali, na heshima, na hata katika dini. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na shikamaneni kwa Kamba ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja wala msifarikiane." Na akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na ikiwa makundi mawili katika Waumini yanapigana, basi yapatanisheni. Na likiwa moja la hao linalidhulumu lingine, basi lipigeni linalo dhulumu mpaka lirejee kwenye amri ya Mwenyezi Mungu..." hadi mwisho wa Aya, na Mtukufu kasema: "Na suluhu ni bora." Na mwenye kujitahidi katika kuwasuluhisha watu ni bora kuliko yule ambaye ni mtiifu katika sala, na saumu, na sadaka. Na mpatanishaji ni lazima Mungu atamfanyia vizuri juhudi zake na matendo yake; kama vile mwenye kufanya juhudi katika kusababisha uharibifu, Mwenyezi Mungu hamfanyii matendo yake kuwa mazuri, wala hafikii makusudio yake. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu: "Hakika Mwenyezi Mungu haitengenezi kazi ya waharibifu." Na mambo haya popote yanapofanywa; basi hayo ni mazuri; kama linavyoonyeshwa hilo kuyatoa katika hukumu ile, lakini ukamilifu wa malipo na utimilifu wake ni kulingana na nia na kumkusudia Mwenyezi Mungu peke yake. Na ndiyo maana akasema: "Na mwenye kufanya hayo kwa kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu, basi tutampa ujira mkubwa." Kwa hivyo, mja anapaswa kukusudia uso wa Mwenyezi Mungu na amfanyie Mwenyezi Mungu peke yake matendo katika kila wakati, na katika kila kipengele miongoni mwa vipengele vya wema. Ili apate kwa hilo ujira mkubwa na ili apate kuzoea kumfanyia Yeye peke yake, ili awe miongoni mwa wenye ikhlasi. Na ili atimiziwe malipo, sawa iwe lengo lake lilitimizwa au hapana. Kwa sababu nia ilipatikana, na yakaambatana nayo yale yanayowezekana miongoni mwa matendo.