Langkau ke kandungan
Tafsir As-Saadi - Swahili · An-Nisaa
Surah 4

An-Nisaa

Ini ialah terjemahan Tafsir as-Saʿdī seperti yang diterbitkan oleh IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca daripada halaman-halaman laman itu. Laman itu tidak menyatakan siapa yang menterjemahkannya atau edisi cetakan mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan syarat untuk mengambil teksnya, maka hak untuk memaparkannya belum disahkan. Belum ada sesiapa yang membandingkannya dengan buku bercetak, dan tiada ulama yang menyemaknya. Setiap bahagian berada di sisi ayat-ayat yang diulasnya, iaitu teks Al-Quran daripada Tanzil, dipaparkan seperti yang ada di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh laman itu berada bersama bahagian sebelumnya, dan indeks menamakan setiap ayat sedemikian. Sabīl tidak menulis atau menterjemahkan satu pun daripadanya.

Teks daripadasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil pada 2026-10-22

Ayat 101

وَإِذَا ضَرَبْتُمْ فِى ٱلْأَرْضِ فَلَيْسَ عَلَيْكُمْ جُنَاحٌ أَن تَقْصُرُوا۟ مِنَ ٱلصَّلَوٰةِ إِنْ خِفْتُمْ أَن يَفْتِنَكُمُ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓا۟ ۚ إِنَّ ٱلْكَـٰفِرِينَ كَانُوا۟ لَكُمْ عَدُوًّا مُّبِينًا 101

{101} Aya mbili hizi ndizo msingi wa ruhusa ya kufupisha swala na swala ya khofu. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu, “Na mnaposafiri katika nchi” yani mnapokuwa katika safari. Na maana ya dhahiri ya Aya ni kwamba inahitaji kuchukua ruhusa hiyo katika safari yoyote ile, hata ikiwa ni safari ya maasia, kama lilivyo dhehebu la Abu Hanifa, Mwenyezi Mungu amrehemu. Na alihalifiwa na walio wengi, yani wale maimamu watatu na wengineo. Hawakuruhusu kuchukua ruhusa hii katika safari ya maasia, wakiifanya Aya hii kuwa mahususi kwa kutumia maana na ufaafu. Kwani, ruhusa ni urahisishaji kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa waja wake wanaposafiri, kwamba wafupishe swala na wasifunge saumu. Naye muasi katika safari yake hali yake haifailii kumfanyia wepesi. Na kauli yake, “basi hakuna ubaya juu yenu mkifupisha Swala.” Yani hakuna ubaya wala dhambi juu yenu katika hilo, na wala hili halipingani na ukweli kwamba kufupisha ndiyo bora zaidi. Kwa sababu, katika kukanusha ubaya kuna kunaondoa baadhi ya fikira potofu iliyomo katika nyingi ya nafsi, na hata halipingani na wajibu wake, kama lilivyotangulia hilo katika Surat Al-Baqara katika kauli yake. “Hakika Swafa na Marwa ni katika alama za Mwenyezi Mungu...” mpaka mwisho wa Aya. Na kuondolewa fikira potofu katika hili ni dhahiri; kwa sababu swala imeshathibiti kwa Waislamu kuwa ni wajibu kwa namna hii kamili. Na wala hili haliwezi kuondolewa katika nafsi za wengi wao isipokuwa kwa kutaja yale yanayopingana nalo. Na ubora wa kufupisha swala juu ya kuikamilisha unaashiriwa na mambo mawili. Moja yake ni kushikamana kwake Nabii – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – na kufupisha katika safari zake zote. Ya pili ni kwamba hili suala ni katika mlango wa kupanua, na kupeana ruhusa, na rehema kwa waja. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu anapenda kwamba zifanywe ruhusa zake kama vile anavyochukia kwamba yafanywe maasia yake. Na kauli yake, “mkifupisha katika Swala” na wala hakusema, ‘mkifupisha Swala’ kwa sababu kuna faida mbili. Ya kwanza ni kwamba kama angesema, ‘mkifupisha Swala’ basi kufupisha huko hakungezuiliwa na mipaka yoyote. Na huenda ingefikiriwa kwamba kama akifupisha sehemu kubwa ya Swala na akaifanya kuwa rakaa moja, kwamba hilo lingetosheleza. Basi kutumia kauli yake, “katika swala” ili iashirie kwamba kufupisha huko kuna mipaka na kumepimwa, na hilo linarudishwa kwa yale aliyowekewa kutokana na matendo ya Nabii – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – na maswahaba zake. Ya pili ni kwamba ‘katika’ inaonyesha kuwa ni baadhi tu, ili ifahamike kwa hilo kuwa kufupisha ni katika baadhi ya Swala za faradhi, na siyo zote. Kwani, Alfajiri na Maghrib hazifupishwi, bali swala zinazofupishwa ni Swala za rakaa nne kutoka rakaa nne hadi mbili. Na inapothibiti kwamba kufupisha katika safari ni ruhusa, basi jua kuwa wafasiri wamehitalifiana kuhusiana na kizuizi hiki, ambacho ni kauli yake, “iwapo mnachelea kwamba wale waliokufuru watawajaribu.” Ambayo maana yake ya dhahiri inaashiria kuwa kufupisha hakuruhusiwi isipokuwa kwa kuwepo kwa mambo mawili haya yote; safari pamoja na hofu. Na jumla ya hitilafu yao inarudi kwa je, kinachomaanishwa na kauli yake, “mkifupisha” ni kufupisha idadi tu au kufupisha idadi na namna? Kwa hivyo, tatizo linakuwa tu katika maana ya kwanza tu. Na hili lilimkanganya Amirul-Muuminina Omar bin al-Khattab, Mwenyezi Mungu amwiye radhi, mpaka akamuuliza Nabii – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – juu ya hilo. Akasema, “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Tuna nini tunafupisha swala ilhali tumekwisha pata amani? Na Mwenyezi Mungu anasema, “iwapo mnachelea kwamba wale waliokufuru watawajaribu.” Mtume wa Mwenyezi Mungu – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – amesema, “Ni sadaka ambayo Mwenyezi Mungu ameitoa juu yenu. Basi ipokeeni sadaka yake.” Au kama alivyosema. Kwa hivyo, kinakuwa kizuizi hiki kililetwa kwa kuzingatia wingi wa hali ambayo walikuwa nayo Nabii – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – na maswahaba zake. Kwani, safari zake nyingi zilikuwa ni safari za Jihadi. Na ina faida nyingine: Nayo ni kuelezea hekima na masilahi yaliyo katika kuweka sheria ya ruhusa ya kufupisha. Akabainisha katika Aya hii ugumu mkubwa zaidi inayofikiriwa ifaayo kuwekewa ruhusa, nayo kujumuika kwa pamoja safari na hofu. Na hilo halilazimu kwamba afupishe wakati wa safari peke yake, ambayo ni mahali penye uwezekano mkubwa wa kuwa na ugumu. Na ama kwa maana ile ya pili, ambayo ni kwamba kinachomaanishwa na kufupisha [hapa] ni kufupisha idadi na namna. Kwa maana, kizuizi hiki kiko kwenye maana yake ya asili. Kwa hivyo, vinapopatikana safari na hofu, inaruhusika kufupisha idadi na kufupisha namna. Na ikipatikana safari peke yake, inaruhusika kupunguza idadi tu, au ikiwa kuna hofu peke yake, basi inaruhusika kufupisha namna peke yake.