Langkau ke kandungan
Tafsir As-Saadi - Swahili · As-Saaffaat
Surah 37

As-Saaffaat

Ini ialah terjemahan Tafsir as-Saʿdī seperti yang diterbitkan oleh IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca daripada halaman-halaman laman itu. Laman itu tidak menyatakan siapa yang menterjemahkannya atau edisi cetakan mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan syarat untuk mengambil teksnya, maka hak untuk memaparkannya belum disahkan. Belum ada sesiapa yang membandingkannya dengan buku bercetak, dan tiada ulama yang menyemaknya. Setiap bahagian berada di sisi ayat-ayat yang diulasnya, iaitu teks Al-Quran daripada Tanzil, dipaparkan seperti yang ada di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh laman itu berada bersama bahagian sebelumnya, dan indeks menamakan setiap ayat sedemikian. Sabīl tidak menulis atau menterjemahkan satu pun daripadanya.

Teks daripadasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil pada 2026-10-22

Ayat 50–59

فَأَقْبَلَ بَعْضُهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ يَتَسَآءَلُونَ 50 قَالَ قَآئِلٌ مِّنْهُمْ إِنِّى كَانَ لِى قَرِينٌ 51 يَقُولُ أَءِنَّكَ لَمِنَ ٱلْمُصَدِّقِينَ 52 أَءِذَا مِتْنَا وَكُنَّا تُرَابًا وَعِظَـٰمًا أَءِنَّا لَمَدِينُونَ 53 قَالَ هَلْ أَنتُم مُّطَّلِعُونَ 54 فَٱطَّلَعَ فَرَءَاهُ فِى سَوَآءِ ٱلْجَحِيمِ 55 قَالَ تَٱللَّهِ إِن كِدتَّ لَتُرْدِينِ 56 وَلَوْلَا نِعْمَةُ رَبِّى لَكُنتُ مِنَ ٱلْمُحْضَرِينَ 57 أَفَمَا نَحْنُ بِمَيِّتِينَ 58 إِلَّا مَوْتَتَنَا ٱلْأُولَىٰ وَمَا نَحْنُ بِمُعَذَّبِينَ 59

{50 - 59} Mwenyezi Mungu Mtukufu alipotaja neema yao na furaha yao kamili kwa vyakula, vinywaji, wenza wao wa kindoa wazuri, na vikao vyao vizuri; akataja kukumbuka kwao wao kwa wao na mazungumzo yao kuhusu mambo yaliyopita, na kwamba waliendelea na mazungumzo hayo na kuulizana mpaka ikapelekea mmoja wao kusema: "Hakika mimi nilikuwa na mwenza katika dunia, na alikuwa akikanusha kufufuliwa na kunilaumu kwamba mimi niliamini hilo, na akawa ananiambia: 'Hivyo wewe ni katika wanaosadiki?' Ati tukishakufa, tukawa udongo na mafupa, ndiyo tutalipwa na kuhesabiwa juu ya matendo yetu?" 'Vipi unasadiki jambo hili lisilowezekana, ambalo linashangaza sana, ambalo ni kwamba tutakapokatikakatika tukawa udongo na mifupa, kwamba tutafufuliwa na kurudishwa, kisha tufanyiwe hesabu na kulipwa juu ya matendo yetu?' Basi huyo mmoja wao akawaambia ndugu zake: Hiki ndicho kisa changu kilichotokea kati yangu na mwenzangu huyo. Mimi bado niliendelea kuamini na kusadiki hayo, naye akaendelea kukadhibisha na kupinga kufufuliwa, mpaka tukafa, tukafufuliwa. Kwa hivyo nikafikia mnayoyaona haya ya neema ambayo Mitume waliyotuambia juu yake, na hapana shaka kuwa ameifikia adhabu yake. Basi "je, nyie mnawaona?" Ili tumwangalie kwa macho na tufurahie zaidi na kuridhika na haya tuliyomo. Kilicho dhahiri hapa kulingana na hali ya watu wa Peponi na furaha yao baina yao na mapatano yao baina yao ni kwamba, walimuitikia katika hayo aliyoyasema, na wakamfuata ili waende wamuone huyo mwenziwe. "Basi atachungulia amwone katikati ya Jahannamu." Yaani, katikati ya adhabu na vilindi vyake. Na adhabu ilikuwa imemzunguka. Basi akamwambia akimlaumu kwa hali yake, na akamshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema zake za kumuokoa kutokana na vitimbi vyake: "Wallahi! (Naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu) Ulikaribia mno kunipoteza," kwa sababu ya utata na fikira potofu ulizoniingiza kwa madai yako yale. "Na lau kuwa si neema ya Mola wangu Mlezi" kwa kunifanya niwe imara katika Uislamu, "bila ya shaka ningelikuwa miongoni mwa waliohudhurishwa" katika adhabu pamoja nawe. "Je, sisi hatutakufa? Isipokuwa kifo chetu cha kwanza? Wala sisi hatutaadhibiwa?" Haya aliyasema huyo Muumini akifurahia neema za Mwenyezi Mungu juu ya watu wa Peponi kwa kuwapa uzima wa milele na kuwasalimisha kutokana na adhabu. Na pia ni swali linalomaanisha uthibitisho wa mambo hayo. Na kauli yake: "Wataelekeana kuulizana wenyewe kwa wenyewe," hapa kimefutwa kile watakachoulizana juu yake, ila mambo yanayotajwa hapa ni ya furaha. Basi hilo likaashiria mambo ambayo wanafurahia kuyazungumzia na masuala ambayo yalikuwa ya mgongano na utata. Inajulikana vyema kwamba raha ya watu wenye elimu katika kuulizana juu ya elimu na kuitafuta inazidi raha iliyopo katika mazungumzo ya kidunia. Watakuwa na sehemu kubwa katika aina hii ya mambo, na watafunuliwa mambo mbalimbali ya uhakika ya kielimu huko Peponi ambayo hayawezi kuelezwa.