Langkau ke kandungan
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Furqaan
Surah 25

Al-Furqaan

Ini ialah terjemahan Tafsir as-Saʿdī seperti yang diterbitkan oleh IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca daripada halaman-halaman laman itu. Laman itu tidak menyatakan siapa yang menterjemahkannya atau edisi cetakan mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan syarat untuk mengambil teksnya, maka hak untuk memaparkannya belum disahkan. Belum ada sesiapa yang membandingkannya dengan buku bercetak, dan tiada ulama yang menyemaknya. Setiap bahagian berada di sisi ayat-ayat yang diulasnya, iaitu teks Al-Quran daripada Tanzil, dipaparkan seperti yang ada di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh laman itu berada bersama bahagian sebelumnya, dan indeks menamakan setiap ayat sedemikian. Sabīl tidak menulis atau menterjemahkan satu pun daripadanya.

Teks daripadasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil pada 2026-10-22

Ayat 42

إِن كَادَ لَيُضِلُّنَا عَنْ ءَالِهَتِنَا لَوْلَآ أَن صَبَرْنَا عَلَيْهَا ۚ وَسَوْفَ يَعْلَمُونَ حِينَ يَرَوْنَ ٱلْعَذَابَ مَنْ أَضَلُّ سَبِيلًا 42

{42} Na ndiyo maana wakasema, "Kwa hakika alikuwa karibu zaidi" [mwanamume huyu] "kutupoteza tuiache miungu yetu" kwa kuifanya miungu kuwa ni mungu mmoja, "lau kuwa hatukushikamana nayo kwa kuvumilia," basi angetupoteza. Walidai, - na Mwenyezi Mungu awaangamize, - kwamba upotovu ndio kumpwekesha Mwenyezi Mungu, na kwamba uwongofu ndio hayo wayafanyayo wao ya ushirikina, na ndiyo maana wakausiana kuendelea kuvumilia juu yake. "Na wakaondoka wakubwa wao wakiwaambia: Nendeni zenu na dumuni na miungu yenu kwa uvumilivu," na hapa wakasema, "lau kuwa hatukushikamana nayo kwa kuvumilia." Na uvumilivu unasifiwa katika kila mahali, isipokuwa mahali hapa. Kwa maana huko ni kuvumilia juu ya sababu za hasira, na juu ya kukithirisha kuni za Jahannamu. Na ama waumini, basi wao ni kama Mwenyezi Mungu alivyosema juu yao, "na wakausiana kwa haki, na wakausiana kusubiri." Na pindi walipohukumu hivi kwamba wao ndio waongofu, na kwamba Mtume ni mpotofu, na ikawa imeshafikia kiwango kwamba hakuna cha kuwasaidia kwacho kufikia uwongofu, akawatishia kwa adhabu, na akawajulisha kwamba wao wakati huo, "watakapoiona adhabu" watajua elimu ya uhakika "ni nani aliyepotea zaidi njia." "Na siku ambayo mwenye kudhulumu atajiuma mikono yake, na huku anasema: Laiti ningelishika njia pamoja na Mtume..." hadi mwisho wa Aya hizi.