An-Noor
Ini ialah terjemahan Tafsir as-Saʿdī seperti yang diterbitkan oleh IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca daripada halaman-halaman laman itu. Laman itu tidak menyatakan siapa yang menterjemahkannya atau edisi cetakan mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan syarat untuk mengambil teksnya, maka hak untuk memaparkannya belum disahkan. Belum ada sesiapa yang membandingkannya dengan buku bercetak, dan tiada ulama yang menyemaknya. Setiap bahagian berada di sisi ayat-ayat yang diulasnya, iaitu teks Al-Quran daripada Tanzil, dipaparkan seperti yang ada di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh laman itu berada bersama bahagian sebelumnya, dan indeks menamakan setiap ayat sedemikian. Sabīl tidak menulis atau menterjemahkan satu pun daripadanya.
Teks daripadasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil pada 2026-10-22
وَٱلَّذِينَ يَرْمُونَ أَزْوَٰجَهُمْ وَلَمْ يَكُن لَّهُمْ شُهَدَآءُ إِلَّآ أَنفُسُهُمْ فَشَهَـٰدَةُ أَحَدِهِمْ أَرْبَعُ شَهَـٰدَٰتٍۭ بِٱللَّهِ ۙ إِنَّهُۥ لَمِنَ ٱلصَّـٰدِقِينَ 6 وَٱلْخَـٰمِسَةُ أَنَّ لَعْنَتَ ٱللَّهِ عَلَيْهِ إِن كَانَ مِنَ ٱلْكَـٰذِبِينَ 7
Badala yake, ushuhuda wa mume dhidi ya mke wake ulimlinda dhidi ya adhabu. Kwa sababu ni jambo la kawaida kwa mume kutomkashifu mke wake ambaye kuingia dosari na uchafu kwake hutokana yale yanayomchafua yeye mkewe isipokuwa yeye ni mkweli, na kwa kuwa anayo haki ya kufanya hivyo, na kwa kuhofia kuambatanisha naye watoto wasio wake, na kwa hukumu zingine zinazokosekana kwa mwengine. Kwa hivyo alisema:
{6-7} "Na wale wanaowasingizia wake zao"; Yaani, wake walio huru wala si wajakazi, "Na hawana," kwa tuhuma zao hizo "Mashahidi ila nafsi zao" kwa sababu hawakusimamisha mashahidi kwa yale waliyokuwa wakiwatuhumu, "Basi ushahidi wa mmoja wao utakuwa kushuhudilia mara nne kwa kiapo cha Mwenyezi Mungu ya kwamba hakika yeye ni katika wasema kweli." Aliuita ushuhuda kwa sababu ni badala ya mashahidi, kwa kusema: Nashuhudia kwa Mwenyezi Mungu kwamba mimi ni miongoni mwa wakweli katika yale niliyomtuhumu juu yake. "Na mara ya tano kwamba laana ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake ikiwa ni miongoni mwa waongo." Yaani, anaongeza ya tano kwa ushahidi uliotangulia, akithibitisha na kutilia mkazo ushahidi huo kwa kujiombea alaaniwe ikiwa ni mwongo. Na ukitimia uombaji wa laana yake; humwondokea yeye adhabu ya kashfa. Yaani, haisimamishwi hukumu ya kashfa juu yake. Maana ya wazi ya Aya ni kwamba, kama atamtaja mtu aliyemtuhumu, basi hakika humwondokea na hupoteza haki yake kwa kufuatia hilo. Je, itasimamishwa adhabu juu yake mke huyo kwa sababu tu ya laana ya mwanaume huyo na kumkataa kwake, au atafungwa? Kuna kauli mbili za wanavyuoni kuhusu hilo. Na ile ambayo dalili inaonyesha ni kwamba itasimamishwa juu yake adhabu, kwa dalili ya kauli yake, “Na mke itamwondokea adhabu kwa kutoa shahada..." hadi mwisho wa aya hiyo. Na lau kama isingekuwa adhabu hiyo ambayo aadhibiwe kwayo mke imelazimika na kutokana na laana ya mume; basi laana ya mke huyo isingezuia lolote katika adhabu hiyo.