Langkau ke kandungan
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Baqara
Surah 2

Al-Baqara

Ini ialah terjemahan Tafsir as-Saʿdī seperti yang diterbitkan oleh IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca daripada halaman-halaman laman itu. Laman itu tidak menyatakan siapa yang menterjemahkannya atau edisi cetakan mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan syarat untuk mengambil teksnya, maka hak untuk memaparkannya belum disahkan. Belum ada sesiapa yang membandingkannya dengan buku bercetak, dan tiada ulama yang menyemaknya. Setiap bahagian berada di sisi ayat-ayat yang diulasnya, iaitu teks Al-Quran daripada Tanzil, dipaparkan seperti yang ada di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh laman itu berada bersama bahagian sebelumnya, dan indeks menamakan setiap ayat sedemikian. Sabīl tidak menulis atau menterjemahkan satu pun daripadanya.

Teks daripadasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil pada 2026-10-22

Ayat 165–167

وَمِنَ ٱلنَّاسِ مَن يَتَّخِذُ مِن دُونِ ٱللَّهِ أَندَادًا يُحِبُّونَهُمْ كَحُبِّ ٱللَّهِ ۖ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ أَشَدُّ حُبًّا لِّلَّهِ ۗ وَلَوْ يَرَى ٱلَّذِينَ ظَلَمُوٓا۟ إِذْ يَرَوْنَ ٱلْعَذَابَ أَنَّ ٱلْقُوَّةَ لِلَّهِ جَمِيعًا وَأَنَّ ٱللَّهَ شَدِيدُ ٱلْعَذَابِ 165 إِذْ تَبَرَّأَ ٱلَّذِينَ ٱتُّبِعُوا۟ مِنَ ٱلَّذِينَ ٱتَّبَعُوا۟ وَرَأَوُا۟ ٱلْعَذَابَ وَتَقَطَّعَتْ بِهِمُ ٱلْأَسْبَابُ 166 وَقَالَ ٱلَّذِينَ ٱتَّبَعُوا۟ لَوْ أَنَّ لَنَا كَرَّةً فَنَتَبَرَّأَ مِنْهُمْ كَمَا تَبَرَّءُوا۟ مِنَّا ۗ كَذَٰلِكَ يُرِيهِمُ ٱللَّهُ أَعْمَـٰلَهُمْ حَسَرَٰتٍ عَلَيْهِمْ ۖ وَمَا هُم بِخَـٰرِجِينَ مِنَ ٱلنَّارِ 167

Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema:

(165, 166, 167) Ni uzuri ulioje wa kuiunganisha Aya hii na ile ya kabla yake. Kwani Yeye Aliyetukuka alipobainisha upweke wake na dalili zake wa zisizokuwa na shaka. Na hoja zake zenye kung'aa na zilizounganishwa na elimu yenye yakini, yenye kuondoa kila shaka. Akataja hapa kwamba “na katika watu” pamoja na huku kubainisha kukamilifu kuna wale wanaomfanyia Mwenyezi Mungu waungu kutoka kwa viumbe. Yani wanamfanyia visawe, na mifano wakiwafanya sawa Mwenyezi Mungu katika ibada, upendo, utukufu na utiifu. Na yule ambaye yuko katika hali hii - baada ya kusimamishiwa hoja na kubainishiwa Tauhidi, - atajulikana kwamba yeye ni mkaidi na mpinzani kwa Mwenyezi Mungu. Au anayekupa mgongo kutafakari Aya zake na kufikiria katika viumbe vyake. Basi yeye hana udhuru hata kidogo katika hilo, bali neno la adhabu limekwisha thibiti juu yake.Na hao ambao wanachukua wenza pamoja na Mwenyezi Mungu hawawafanyi kuwa sawa na Mwenyezi Mungu katika uumbaji, riziki na kupanga mambo. Bali wanawafanya kuwa sawa naye katika ibada, na wanawaabudu ili wawaweke karibu naye. Na katika kauli yake “walijifanyia (waungu)” ni dalili ya kwamba Mwenyezi Mungu hana mwenza, lakini washirikina ndio waliowafanya baadhi ya viumbe kuwa wenza wake. Jina la dhahania tu, na neno lisilokuwa na maana, kama alivyosema Mtukufu: “Na wamemfanyia Mwenyezi Mungu washirika! Sema: Watajeni. Au ndio mnampa habari ya yale asiyoyajua katika ardhi, au ni maneno matupu?” [Na kauli yake:] “Hayo hayakuwa isipokuwa ni majina mliyowapa nyinyi na baba zenu. Mwenyezi Mungu hakuleta uthibitisho wowote juu ya hayo. Hawafuati isipokuwa dhana tu.” Kwa hivyo, kiumbe hakilingani na Mwenyezi Mungu kwa sababu Mwenyezi Mungu ndiye Muumba, na visivyokuwa yeye vimeumbwa. Na Mola Mlezi ndiye Mwenye kuruzuku, nao wasiokuwa yeye wanaruzukiwa. Na Mwenyezi Mungu ndiye anayejitosheleza, nanyi ndio masikini. Naye ndiye mkamilifu kwa namna zote, nao waja ni wapungufu kwa namna zote. Na Mwenyezi Mungu ndiye mwenye kunufaisha, mwenye kudhuru, nao viumbe hawana chochote katika kunufaisha na kudhuru na amri. Basi akajulikana elimu ya yakini ubatili wa kauli ya aliyejichukulia miungu na wenza badala ya Mwenyezi Mungu. Sawa awe mfalme au nabii, au mwema, au sanamu, au visivyokuwa hivyo. Na kwamba Mwenyezi Mungu ndiye anayestahili upendo kamili na unyenyekevu kamili. Ndio maana Mwenyezi Mungu akawasifu Waumini kwa kauli yake: “Lakini walioamini wanampenda Mwenyezi Mungu zaidi sana.” Yani kushinda (upendo wa) hao wafanyao wenza kwa wenza wao. Kwa kuwa wao (Waumini) walimfanyia yeye tu mapenzi yao, nao hao waliwashirikisha hao wenza. Na kwa sababu (Waumini) walimpenda yule anayestahiki kupendwa kwa hakika. Ambaye kumpenda ndio kutengenea hasa kwa mja na furaha yake na kufaulu kwake. Nao washirikina waliwapenda wasiostahiki chochote katika mapenzi. Na kuwapenda ndio upotofu wenyewe na uharibifu wake, na kutawanyika kwa mambo yake. Ndio maana Mwenyezi Mungu akawatishia kwa kauli yake: “Na lau waliodhulumu wakajua,” kwa kumchukulia (Mwenyezi Mungu) wenza na kumfuata asiyekuwa Mola Mlezi wa waja. Na wakawadhulumu viumbe kwa kuwazuilia njia ya Mwenyezi Mungu, na kujitahidi kwao katika yale yanayowadhuru. “Watakapoiona adhabu,” yani Siku ya Kiyama kwa macho yao waziwazi, “kuwa nguvu zote ni za Mwenyezi Mungu na kuwa Mwenyezi Mungu ni mkali wa kuadhibu!” Yani wangelijua kujua kwa uthabiti kwamba nguvu na uwezo wote ni wa Mwenyezi Mungu. Na kwamba hao wenza wao hawana nguvu yoyote. Basi ikawabainikia katika siku hiyo udhaifu wao (hao wenza) na upungufu wao. Kama walivyowachanganya katika dunia na wakadhania kuwa wana kitu katika hilo jambo, na kwamba wanawaweka karibu kwake (Mwenyezi Mungu) na wanawafikisha kwake. Lakini, ikahasirika dhana yao, na juhudi zao zikawa bure, na ukali wa adhabu ukastahiki juu yao; na wenza wao hawakuzuilia chochote. Na hawakuwafaa hata chembe ya sisimizi ya manufaa, bali wanapata madhara kutoka kwao, ilhali walidhani kuwa watawanufaisha. Na wanaofuatwa wakawatenga wafuasi wao, na mafungamano ambayo yalikuwa kati yao duniani yatakatika. Kwa sababu yalikuwa kwa ajili ya asiyekuwa Mwenyezi Mungu, na juu ya isiyokuwa amri ya Mwenyezi Mungu, na wanayohusiana na batili ambayo haina uhakika wowote. Basi matendo yao yakapotelea mbali, na hali zao zikaangamia, na ikawadhihirikia kuwa wao walikuwa ni waongo.Na kwamba matendo yao waliyoyatarajia yawanufaishe na wapate matokeo yake yaliwabadilikia kuwa masikitiko na majuto. Na kwamba watadumu ndani ya Moto milele wala hawatatoka humo abadani. Basi je baada ya hasara hii kuna hasara nyingine? Hilo ni kwa sababu walifuata batili, hivyo wakafanya matendo batili, na wakataraji jambo lisilotarajiwa. Na wakashikamana na lisiloshikamanwa nalo, basi matendo yao yakabatilika kwa sababu ya kubatilika kwa kile yaliyoshikamana nacho. Na (matendo yao) yalipobatilika, wakapata kusikitika juu ya matumaini waliyokosa ndani yake, kwa hivyo yakawadhuru kudhuru kukubwa mno. Hili ni tofauti na aliyeshikamana na Mwenyezi Mungu, Mfalme wa haki iliyo wazi. Na akaufanyia uso wake tu matendo, na akatarajia manufaa yake. Basi huyu bila shaka aliiweka haki mahali pake. Kwa hivyo matendo yake yakawa haki, kwa sababu ya kushikamana kwake na haki, basi akafaulu kupata matokeo ya matendo yake. Na akakuta malipo yake yasiyokatika kwa Mola wake Mlezi, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu “1. Waliokufuru na wakazuilia njia ya Mwenyezi Mungu, Yeye atavipotoa vitendo vyao. 2. Na walioamini, na wakatenda mema, na wakaamini aliyoteremshiwa Muhammad - nayo ni Haki iliyotoka kwa Mola wao Mlezi -, atawafutia makosa yao na ataitengeneza hali yao. 3. Hayo ni kwa sababu, waliokufuru wamefuata upotovu, na walioamini wamefuata Haki iliyotoka kwa Mola wao Mlezi. Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu anavyowapigia watu mifano yao.” Na wakati huo, wafuasi watatamani kwamba warudishwe duniani, ili wajitenge na wale ambao wao waliwafuata kwa kuacha kumshirikisha Mwenyezi Mungu. Na waelekee kwenye kumfanyia Mwenyezi Mungu tu matendo. Lakini, ni mbali mno vipi hilo! Jambo hilo (wanalotaka) limeshapita, na huu wakati siyo wakati wa kupewa muhula. Na pamoja na hayo, wao ni waongo, kwa maana wangelirudishwa bila ya shaka wangeyarejea yale waliyokatazwa. Lakini hiyo ni kauli wanayosema tu, na matamanio tu wanayotamani, kwa sababu ya ghadhabu kubwa juu ya wale ambao wao waliwafuata walipojitenga nao, ijapokuwa lawama ni zao. Na kichwa cha wale wanaofuatwa katika uovu ni Shetani, na licha ya hayo, anawaambia wafuasi wake wakati itakapokatwa hukumu. “Hakika, Mwenyezi Mungu alikuahidini ahadi ya kweli. Nami nilikuahidini; lakini sikukutimizieni. Na sikuwa na mamlaka juu yenu, isipokuwa kwamba nilikuiteni, nanyi mkaniitikia. Basi msinilaumu mimi, bali jilaumuni wenyewe.”