Langkau ke kandungan
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Baqara
Surah 2

Al-Baqara

Ini ialah terjemahan Tafsir as-Saʿdī seperti yang diterbitkan oleh IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca daripada halaman-halaman laman itu. Laman itu tidak menyatakan siapa yang menterjemahkannya atau edisi cetakan mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan syarat untuk mengambil teksnya, maka hak untuk memaparkannya belum disahkan. Belum ada sesiapa yang membandingkannya dengan buku bercetak, dan tiada ulama yang menyemaknya. Setiap bahagian berada di sisi ayat-ayat yang diulasnya, iaitu teks Al-Quran daripada Tanzil, dipaparkan seperti yang ada di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh laman itu berada bersama bahagian sebelumnya, dan indeks menamakan setiap ayat sedemikian. Sabīl tidak menulis atau menterjemahkan satu pun daripadanya.

Teks daripadasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil pada 2026-10-22

Ayat 163

وَإِلَـٰهُكُمْ إِلَـٰهٌ وَٰحِدٌ ۖ لَّآ إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ٱلرَّحْمَـٰنُ ٱلرَّحِيمُ 163

Mwenyezi Mungu Mtukufu anatoa habari - na Yeye ndiye mkweli zaidi wa wasemao – kwamba Yeye, “ni Mungu mmoja tu.” Yani Mpweke, Mmoja tu dhati yake, majina yake, sifa zake, na vitendo vyake. Hana mshirika yeyote katika dhati yake, wala mwenye jina kama lake, wala anayelingana naye, wala mfano wake, wala aliye sawa naye, wala Muumba, wala Mwendeshaji isipokuwa Yeye. Na ikiwa ni hivyo, basi Yeye ndiye anayestahiki kufanyiwa uungu na kuabudiwa kwa kila aina za ibada. Na asishirikishwe yeyote pamoja naye katika viumbe vyake, kwa sababu Yeye ni, “Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.” Anayesifika kwa rehema kubwa ambayo haifanani nayo rehema ya yeyote yule. Kwa maana, (rehema zake) zimeenea na kujumuisha kila kilicho hai. Na kwa rehema yake, viumbe vilipatikana, na kwa rehema yake vilipata aina za vyakula. Na kwa rehema yake kila mateso, na kwa rehema zake aliwajulisha waja wake nafsi yake kwa sifa zake na neema zake. Na akawabainishia kila wanalohitaji katika masilahi ya dini yao na dunia yao kwa kuwatuma Mitume na kuteremsha Vitabu. Na ikishajulikana kuwa chochote walichonacho waja katika neema ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Na kwamba hakuna mmoja katika viumbe hawezi kumfaidi mwingine, basi anajulikana kuwa Mwenyezi Mungu ndiye anayestahiki ibada za aina zote. Na kwamba Yeye peke yake apendwe, ahofiwe, atumainiwe, atukuzwe, ategemewe, na aina nyingine za utiifu. Na kwamba dhuluma ya dhuluma zote na ubaya wa ubaya wote ni kuacha kumuabudu na kwenda kuwaabudu waja. Na kumshirikisha Mola Mlezi wa mabwana wote na viumbe walioumbwa kutokana na udongo, au kumwabudu kiumbe anayeendeshwa. Asiyekuwa na uwezo kwa namna zote pamoja na Muumba, mwenye kuendesha kila kitu, mwenye uwezo, mwenye nguvu, ambaye [tayari] alikwishashinda kila kitu; na kila kitu kikawa chini ya hukumu yake. Na katika Aya hii, kuna uthibitisho wa upweke wa Muumba mwanzilishi na Uungu wake. Na kutia hilo mkazo kwa kukanusha hilo kutoka kwa asiyekuwa yeye katika viumbe. Na kubainisha asili ya dalili ya hilo, ambayo ni kuthibitisha rehema yake ambayo miongoni mwa athari zake, ni kuwepo kwa neema zote na kuzuilika kwa mateso zote. Basi hii ni dalili ya ujumla juu ya upweke wake Mtukufu. Kisha akataja dalili za kina, akasema: