Al-Baqara
Ini ialah terjemahan Tafsir as-Saʿdī seperti yang diterbitkan oleh IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca daripada halaman-halaman laman itu. Laman itu tidak menyatakan siapa yang menterjemahkannya atau edisi cetakan mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan syarat untuk mengambil teksnya, maka hak untuk memaparkannya belum disahkan. Belum ada sesiapa yang membandingkannya dengan buku bercetak, dan tiada ulama yang menyemaknya. Setiap bahagian berada di sisi ayat-ayat yang diulasnya, iaitu teks Al-Quran daripada Tanzil, dipaparkan seperti yang ada di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh laman itu berada bersama bahagian sebelumnya, dan indeks menamakan setiap ayat sedemikian. Sabīl tidak menulis atau menterjemahkan satu pun daripadanya.
Teks daripadasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil pada 2026-10-22
وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّن مَّنَعَ مَسَـٰجِدَ ٱللَّهِ أَن يُذْكَرَ فِيهَا ٱسْمُهُۥ وَسَعَىٰ فِى خَرَابِهَآ ۚ أُو۟لَـٰٓئِكَ مَا كَانَ لَهُمْ أَن يَدْخُلُوهَآ إِلَّا خَآئِفِينَ ۚ لَهُمْ فِى ٱلدُّنْيَا خِزْىٌ وَلَهُمْ فِى ٱلْـَٔاخِرَةِ عَذَابٌ عَظِيمٌ 114
(114) Yani hakuna yeyote dhalimu mkubwa na mwenye makosa makubwa zaidi kuliko yule anayeizuia misikiti ya Mwenyezi Mungu kutajwa Mwenyezi Mungu ndani yake, na kusimamisha Swala na mengineyo katika [aina za] utiifu. "Na akajitahidi" yani akafanya jitihada kadiri awezavyo "katika kuiharibu." Kihisia na kimaana. Nako kuharibu kwa kihisia ni kuibomoa, kuiharibu, na kuichafua. Nako kuharibu kwa kimaana ni kuzuia wale wanaolitaja jina la Mwenyezi Mungu ndani yake. Na hili ni la jumla kwa kila anayesifika kwa hizo sifa. Kwa hivyo, wanaingia humo wale wenye tembo, na Maquraishi walipomzuia Mtume wa Mwenyezi Mungu katika mwaka wa Hudaybiya. Na Wakristo walipoiharibu Baitul-Maqdis na aina nyinginezo za madhalimu wanaojitahidi katika kuiharibu, wakimpinga Mwenyezi Mungu na kumuasi. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akawalipa kwamba aliwazuia kuingia humo kisheria na kimakadirio isipokuww kwa hofu, wadhalilifu. Basi walipowaogopesha waja wa Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu akawatia hofu. Hivyo, wale washirikina waliomzuia Mtume wake, hakukaa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake isipokuwa kwa muda mfupi tu na Mwenyezi Mungu akamruhusu kuiteka Makka na kuwazuia washirikina kuikaribia nyumba yake. Akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu "Enyi mlioamini! hakika washirikina ni najisi, kwa hivyo wasiukaribie Msikiti Mtukufu baada ya mwaka wao huu." Na wale wenye tembo, Mwenyezi Mungu amekwisha taja yaliyowasibu. Nao Wakristo, Mwenyezi Mungu aliwatia nguvu Waumini juu yao, basi wakawatoa [huko]. Na vivyo hivyo kila anayesifika kwa sifa zao, basi ni lazima apatwe na fungu lake. Na hii ni miongoni mwa Aya (Ishara) kubwa alizozieleza Muumba kabla ya kutokea kwake, hivyo zikatokea kama alivyosema. Na wanachuoni walitumia aya hii tukufu kama hoja kuwa hairuhusiki kuwawezesha makafiri kuingia misikitini. "Duniani watapata hizaya" [yani] yenye fedheha kama ilivyotangulia "na Akhera watapata adhabu kubwa." Na ikiwa hakuna dhalimu mkubwa kuliko yule anayezuia misikiti ya Mwenyezi Mungu kutajwa ndani yake jina lake, basi hakuna mwenye imani kubwa kuliko yule anayejitahidi katika kuiimarisha misikiti; kuimarisha kwa kihisia na kwa kimaana, kama alivyosema Mtukufu. "Anayestawisha misikiti ya Mwenyezi Mungu ni yeye tu amwaminiye Mwenyezi Mungu na Siku ya mwisho." Bali Mwenyezi Mungu Mtukufu aliamrisha nyumba zake zinyanyuliwe, zitukuzwe na ziheshimiwe. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Katika nyumba ambazo Mwenyezi Mungu ameruhusu zinyanyuliwe, na humo litajwe jina lake" Na misikiti ina hukumu nyingi jumla yake inarudi kwa yaliyomo katika Aya hizi tukufu.