Langkau ke kandungan
Tafsir As-Saadi - Swahili · Yusuf
Surah 12

Yusuf

Ini ialah terjemahan Tafsir as-Saʿdī seperti yang diterbitkan oleh IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca daripada halaman-halaman laman itu. Laman itu tidak menyatakan siapa yang menterjemahkannya atau edisi cetakan mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan syarat untuk mengambil teksnya, maka hak untuk memaparkannya belum disahkan. Belum ada sesiapa yang membandingkannya dengan buku bercetak, dan tiada ulama yang menyemaknya. Setiap bahagian berada di sisi ayat-ayat yang diulasnya, iaitu teks Al-Quran daripada Tanzil, dipaparkan seperti yang ada di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh laman itu berada bersama bahagian sebelumnya, dan indeks menamakan setiap ayat sedemikian. Sabīl tidak menulis atau menterjemahkan satu pun daripadanya.

Teks daripadasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil pada 2026-10-22

Ayat 100

وَرَفَعَ أَبَوَيْهِ عَلَى ٱلْعَرْشِ وَخَرُّوا۟ لَهُۥ سُجَّدًا ۖ وَقَالَ يَـٰٓأَبَتِ هَـٰذَا تَأْوِيلُ رُءْيَـٰىَ مِن قَبْلُ قَدْ جَعَلَهَا رَبِّى حَقًّا ۖ وَقَدْ أَحْسَنَ بِىٓ إِذْ أَخْرَجَنِى مِنَ ٱلسِّجْنِ وَجَآءَ بِكُم مِّنَ ٱلْبَدْوِ مِنۢ بَعْدِ أَن نَّزَغَ ٱلشَّيْطَـٰنُ بَيْنِى وَبَيْنَ إِخْوَتِىٓ ۚ إِنَّ رَبِّى لَطِيفٌ لِّمَا يَشَآءُ ۚ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلْعَلِيمُ ٱلْحَكِيمُ 100

{100} "Na akawapandisha wazazi wake kwenye kiti cha enzi,” yaani, juu ya kitanda cha mfalme na kiti mheshimiwa, "Na wote wakaporomoka kumsujudia.” Yaani, baba yake, mama yake, na ndugu zake walimsujudia kwa njia ya taadhima, na heshima na kutukuza. "Na Akasema" alipoona hali hii, na akaona kumsujudia kwao, "Ewe baba yangu! Hii ndiyo tafsiri ya ile ndoto yangu ya zamani” wakati alipoona nyota kumi na moja na jua na mwezi vinamsujudia. Basi hili ndilo kutokea kwake ambako kuliishia na kufikia. "Na Mola wangu Mlezi ameifanya kuwa kweli” na hakuifanya kuwa ndoto zilizochanganyikana. "Na Mwenyezi Mungu amenifanyia uzuri” mkubwa sana “kunitoa gerezani, na akawaleta kutoka jangwani.” Na hili ni katika upole wake na usemi wake mzuri, yeye amani iwe juu yake, ambapo aliitaja hali yake gerezani, lakini hakutaja hali yake ndani ya kisima, kwa sababu ya msamaha wake kamili kwa ndugu zake, na kwamba haitaji dhambi hiyo, na kwamba kuja kwenu kutoka jangwani ni katika ihsan ya mwenyezi Mungu kwangu. Na hakusema aliwatoa katika njaa na uchovu, wala hakusema: Aliwafanyia uzuri. Bali alisema: Alinifanyia uzuri. Kwa hivyo alifanya uzuri kumrudia yeye. Basi ni Mwingi wa baraka anayemteua kwa rehema yake amtakaye katika waja wake na akawatunuku rehema itokayo kwake, hakika Yeye ndiye Mwenye kutunuku "baada ya Shetani kuchochea baina yangu na ndugu zangu.” Na hakusema: Shetani aliwachochea ndugu zangu. Bali badala yake ni kana kwamba dhambi hiyo na ujinga huo umetoka katika pande zote mbili. Basi sifa njema ni zake Mwenyezi Mungu ambaye alimhizi Shetani, akamuweka mbali, na akatuleta pamoja baada ya kutengana huko kugumu. "Hakika Mola wangu Mlezi ni Mpole kwa alitakalo.” Anamfikishia mja wema wake na ihsani yake kutokea mahali asipohisi, na humfikisha katika vyeo vya juu kutoka katika mambo anayoyachukia. "Hakika Yeye ndiye Mwenye kujua vyema” ambaye anajua mambo ya dhahiri na ya ndani na siri na dhamiri za waja wake. “Mwenye hekima” katika kuviweka kwake vitu mahali pake na kuyaleta mambo katika nyakati zake yaliyoandikiwa.