Yunus
Ini ialah terjemahan Tafsir as-Saʿdī seperti yang diterbitkan oleh IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca daripada halaman-halaman laman itu. Laman itu tidak menyatakan siapa yang menterjemahkannya atau edisi cetakan mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan syarat untuk mengambil teksnya, maka hak untuk memaparkannya belum disahkan. Belum ada sesiapa yang membandingkannya dengan buku bercetak, dan tiada ulama yang menyemaknya. Setiap bahagian berada di sisi ayat-ayat yang diulasnya, iaitu teks Al-Quran daripada Tanzil, dipaparkan seperti yang ada di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh laman itu berada bersama bahagian sebelumnya, dan indeks menamakan setiap ayat sedemikian. Sabīl tidak menulis atau menterjemahkan satu pun daripadanya.
Teks daripadasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil pada 2026-10-22
فَلَوْلَا كَانَتْ قَرْيَةٌ ءَامَنَتْ فَنَفَعَهَآ إِيمَـٰنُهَآ إِلَّا قَوْمَ يُونُسَ لَمَّآ ءَامَنُوا۟ كَشَفْنَا عَنْهُمْ عَذَابَ ٱلْخِزْىِ فِى ٱلْحَيَوٰةِ ٱلدُّنْيَا وَمَتَّعْنَـٰهُمْ إِلَىٰ حِينٍ 98
{98} Yeye Mtukufu Anasema: "Basi kwa nini hakikuwepo kijiji" miongoni mwa vijiji vilivyokadhibisha, "kilichoamini" wakati kilipoiona adhabu, "kwa hivyo Imani yake ikakifaa." Yaani, hakuna hata mmoja wao aliyefaidika na imani yake wakati alipoiona adhabu, kama Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyosema hivi karibuni kuhusu Firauni, aliposema, "Nimeamini kuwa hakuna mungu isipokuwa yule ambaye walimwamini Wana wa Israili, na mimi ni miongoni mwa Waislamu." Lakini akaambiwa, "Je, sasa? Na ilhali uliasi kabla yake na ukawa miongoni mwa waharibifu" na kama alivyosema Yeye Mtukufu "basi walipoiona adhabu yetu, wakasema: Tumemuamini Mwenyezi Mungu kuwa ni wa pekee, na tunaikataa miungu tuliyokuwa tukiishirikisha naye. Lakini imani yao haikuwa yenye kuwafaa kitu wakati ambao walipokwisha iona adhabu yetu. Hii ndiyo desturi ya Mwenyezi Mungu ambayo ilikwishatangulia kwa waja wake." Na Yeye Mtukufu akasema: “Mpaka yanapomjia mmoja wao mauti, anasema, "Mola wangu Mlezi! Nirudishe, ili nitende mema sasa badala ya yale niliyoyaacha." Wapi!" Na hekima katika haya iko wazi. Kwani Imani ya kulazimishwa si imani ya kweli. Kwa maana lau yataondolewa kwake adhabu hiyo na jambo ambalo lilimlazimisha kuamini, basi angerudi katika ukafiri. Na kauli yake: "isipokuwa kaumu ya Yunus? Walipoamini, tukawaondolea adhabu ya hizaya katika uhai wa dunia, na tukawastarehesha kwa muda." Basi wao wameondolewa katika ujumla uliotangulia, na lazima hilo ni kwa sababu ya hekima kutoka kwa ajuaye zaidi mambo ya ghaibu na yanayoonekana ambayo haijatufikia na wala ufahamu wetu haukuifikia. Amesema Yeye Mtukufu: "Na hakika Yunus alikuwa miongoni mwa Mitume..." mpaka aliposema: "Na tulimtuma kwa watu laki moja au zaidi. Basi wakaamini, na tukawastarehesha kwa muda." Na pengine hekima katika hilo ni kwamba wasiokuwa wao miongoni mwa wale walioangamizwa lau wangerudishwa, basi wangerejea katika yale waliyokatazwa. Na ama kaumu ya Yunus, hao Mwenyezi Mungu alijua zaidi kwamba imani yao itaendelea, bali iliendelea kihalisi, na wakadumu juu yake. Na Mwenyezi Mungu ndiye anayejua zaidi.