At-Tawba
Ini adalah terjemahan Tafsir as-Saʿdī sebagaimana diterbitkan IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca dari halaman-halaman situs itu. Situs itu tidak menyebutkan siapa yang menerjemahkannya maupun edisi cetak mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan ketentuan untuk mengambil teksnya, sehingga hak untuk menampilkannya belum diverifikasi. Belum ada yang membandingkannya dengan buku cetak, dan belum ada ulama yang meninjaunya. Setiap bagian berdiri di samping ayat-ayat yang diulasnya, yaitu teks Al-Qur’an dari Tanzil, ditampilkan sebagaimana adanya di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh situs itu berdiri bersama bagian sebelumnya, dan indeks menyebutkan setiap ayat semacam itu. Sabīl tidak menulis atau menerjemahkan satu pun darinya.
Teks darisaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil 2026-10-22
وَلَا تُصَلِّ عَلَىٰٓ أَحَدٍ مِّنْهُم مَّاتَ أَبَدًا وَلَا تَقُمْ عَلَىٰ قَبْرِهِۦٓ ۖ إِنَّهُمْ كَفَرُوا۟ بِٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ وَمَاتُوا۟ وَهُمْ فَـٰسِقُونَ 84
{84} Yeye Mtukufu Anasema: "Wala usimsalie kabisa yeyote katika wao akifa" miongoni mwa wanafiki, "wala usisimame kaburini kwake" baada ya kuzikwa ili umuombee dua. Kwa maana kuswali kwake na kusimama kwake kwenye makaburi yao ni uombezi wake kwao, nao uombezi hauwafai kitu. "Hakika hao walimkufuru Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na wakafa na hali ni wamevuka mipaka." Na yule ambaye ni kafiri na akafa katika hali hiyo, basi Uombezi wa waombezi hautamnufaisha kitu. Na katika hilo kuna mazingatia kwa wengineo, na karipio, na adhabu kwao. Na kadhalika kila anayejulikana kuwa na ukafiri na unafiki, basi yeye haswaliwi. Na katika Aya hii kuna ushahidi juu ya sheria ya uhalali wa kuwaswalia Waumini na kusimama kwenye makaburi yao ili kuwaombea dua, kama alivyokuwa Nabii – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – hivyo kwa waumini. Kwa maana, kufungia katazo hili kwa wanafiki kunaonyesha kuwa lilikuwa limethibiti kuhusiana na waumini.