An-Naba
Ini adalah terjemahan Tafsir as-Saʿdī sebagaimana diterbitkan IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca dari halaman-halaman situs itu. Situs itu tidak menyebutkan siapa yang menerjemahkannya maupun edisi cetak mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan ketentuan untuk mengambil teksnya, sehingga hak untuk menampilkannya belum diverifikasi. Belum ada yang membandingkannya dengan buku cetak, dan belum ada ulama yang meninjaunya. Setiap bagian berdiri di samping ayat-ayat yang diulasnya, yaitu teks Al-Qur’an dari Tanzil, ditampilkan sebagaimana adanya di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh situs itu berdiri bersama bagian sebelumnya, dan indeks menyebutkan setiap ayat semacam itu. Sabīl tidak menulis atau menerjemahkan satu pun darinya.
Teks darisaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil 2026-10-22
أَلَمْ نَجْعَلِ ٱلْأَرْضَ مِهَـٰدًا 6 وَٱلْجِبَالَ أَوْتَادًا 7 وَخَلَقْنَـٰكُمْ أَزْوَٰجًا 8 وَجَعَلْنَا نَوْمَكُمْ سُبَاتًا 9 وَجَعَلْنَا ٱلَّيْلَ لِبَاسًا 10 وَجَعَلْنَا ٱلنَّهَارَ مَعَاشًا 11 وَبَنَيْنَا فَوْقَكُمْ سَبْعًا شِدَادًا 12 وَجَعَلْنَا سِرَاجًا وَهَّاجًا 13 وَأَنزَلْنَا مِنَ ٱلْمُعْصِرَٰتِ مَآءً ثَجَّاجًا 14 لِّنُخْرِجَ بِهِۦ حَبًّا وَنَبَاتًا 15 وَجَنَّـٰتٍ أَلْفَافًا 16
Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akataja neema na ushahidi vinavyoonyesha yale waliyoyaleta Mitume, akasema:
{6 - 16} Yaani, je, hatukuneemesheni kwa neema kubwa kubwa, na tukakufanyieni "ardhi kama tandiko" kwa ajili ya masilahi yenu kama vile kupanda mimea na kujenga majumba na kujifanyia njia za kupitia? "Na milima kama vigingi" vya kuishikilia ardhi isije ikavurugika na kuwayumbayumbisha. "Na tukakuumbeni kwa jozi?" Yaani, wanaume na wanawake wa jinsia moja; ili kila mmoja wao apate utulivu katika mwenziwe, na hapo yapatikane mapenzi na huruma, na uzao utokee kutoka kwa hayo. Basi katika hayo kuna ukumbusho juu ya neema ya kufurahia ngono. "Na tukakufanya kulala kwenu ni mapumziko?" Ili kumaliza shughuli zenu nyingi, ambazo ikiwa mtaendelea kuzifanya, zitawadhuru miili yenu. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akaujaalieni usiku na usingizi kuwafunika watu ili harakati zenu zenye madhara zitulie na yapatikane mapumziko yao yenye manufaa kwao. "Na tukajenga juu yenu saba zenye nguvu?" Yaani, mbingu saba zenye nguvu mno na uthabiti, na Mwenyezi Mungu akazishikilia kwa uweza wake, na akazifanya kuwa ni paa la ardhi, ndani yake yamo manufaa mengi kwao, na ndiyo maana akataja jua miongoni mwa manufaa yake, akasema: "Na tukaifanya taa yenye mwanga na joto." Kwa kutaja taa, akawa anaashiria manufaa yake ambayo ni mwangaza, ambao unahitajiwa mno na viumbe, na pia akataja joto lake ambalo linaivusha na pia lina manufaa mengine. "Na tukateremsha maji yanayoanguka kwa kasi kutoka mawinguni. Ili tutoe kwayo nafaka" kama vile ngano, shayiri, mahindi, mchele na vitu vinginevyo wanavyokula wanadamu. "Na mimea" yote ambayo Mwenyezi Mungu ameifanya kuwa ni chakula cha mifugo yao. "Na mabustani yenye miti iliyokamatana" yenye kila aina ya matunda matamu. Kwa hivyo, Yule ambaye amekuneemesheni neema hizi kubwa ambazo thamani yake haina kikomo wala idadi yake haihesabiki, basi vipi mnamkufuru na kumkadhibisha katika yale aliyokuambieni kuhusu kufufuliwa na kutawanywa? Au mnatafutaje msaada kutoka kwa neema zake katika kumuasi na tena mnazikataa?