Langsung ke konten
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Hashr
Surah 59

Al-Hashr

Ini adalah terjemahan Tafsir as-Saʿdī sebagaimana diterbitkan IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca dari halaman-halaman situs itu. Situs itu tidak menyebutkan siapa yang menerjemahkannya maupun edisi cetak mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan ketentuan untuk mengambil teksnya, sehingga hak untuk menampilkannya belum diverifikasi. Belum ada yang membandingkannya dengan buku cetak, dan belum ada ulama yang meninjaunya. Setiap bagian berdiri di samping ayat-ayat yang diulasnya, yaitu teks Al-Qur’an dari Tanzil, ditampilkan sebagaimana adanya di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh situs itu berdiri bersama bagian sebelumnya, dan indeks menyebutkan setiap ayat semacam itu. Sabīl tidak menulis atau menerjemahkan satu pun darinya.

Teks darisaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil 2026-10-22

Ayat 8–9

لِلْفُقَرَآءِ ٱلْمُهَـٰجِرِينَ ٱلَّذِينَ أُخْرِجُوا۟ مِن دِيَـٰرِهِمْ وَأَمْوَٰلِهِمْ يَبْتَغُونَ فَضْلًا مِّنَ ٱللَّهِ وَرِضْوَٰنًا وَيَنصُرُونَ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥٓ ۚ أُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلصَّـٰدِقُونَ 8 وَٱلَّذِينَ تَبَوَّءُو ٱلدَّارَ وَٱلْإِيمَـٰنَ مِن قَبْلِهِمْ يُحِبُّونَ مَنْ هَاجَرَ إِلَيْهِمْ وَلَا يَجِدُونَ فِى صُدُورِهِمْ حَاجَةً مِّمَّآ أُوتُوا۟ وَيُؤْثِرُونَ عَلَىٰٓ أَنفُسِهِمْ وَلَوْ كَانَ بِهِمْ خَصَاصَةٌ ۚ وَمَن يُوقَ شُحَّ نَفْسِهِۦ فَأُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلْمُفْلِحُونَ 9

{8 - 9} Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akataja hekima na sababu kwa nini aliwapa hayo makundi ngawira za vita, na kwamba wao wanastahiki kusaidiwa, wanaostahiki kupewa, na kwamba wao ni miongoni mwa wahamiaji; ambao waliziacha nyumba zao wanazozipenda na walizozizoea, nchi zao, wapenzi wao, wendani wao, na mali zao, kwa ajili ya kumtaka Mwenyezi Mungu, na kuunga mkono dini yake, na kumpenda Mtume wa Mwenyezi Mungu. Hawa ndio wakweli. Wale waliofanya matendo kulingana na Imani yao, na wakaisadikisha Imani yao kwa vitendo vyao vizuri na ibada ngumu; tofauti na wale waliodai kuwa na imani lakini hawakuisadikisha kwa jihadi, kuhama, na ibada nyinginezo, na miongoni mwa Answar, yaani Aws na Khazraj, ambao walimwamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa kutii, kwa mapenzi na hiari, na wakampa kimbilio Mtume wa Mwenyezi Mungu - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - na wakamzuilia mbali na mwekundu na mweusi, na wakaandaa makazi ya kuhamia na imani, mpaka yakawa ni makazi na marejeo ambayo Waumini hurejea, wahamiaji hutafuta hifadhi huko, na Waislamu wanaishi katika hiyama yake. Kwa vile nchi zote zilikuwa nchi za vita, ushirikina, na uovu, lakini wale wanaoinusuru Dini waliendelea tu kutafuta hifadhi kwa Ansari, mpaka Uislamu ukaenea na kuwa na nguvu na ukaanza kuongezeka - kidogo kidogo, [na kukua kidogo kidogo] mpaka wakafungua nyoyo kwa elimu, imani, na Qur-ani, na wakfaungua nchi kwa upanga na mikuki, ambayo miongoni mwa maelezo yao ya mazuri ya jumla ni kuwa wao “wanawapenda wale waliohamia kwao” na hayo ni kwa sababu ya kumpenda kwao Mwenyezi Mungu na Mtume – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – “wala hawaoni choyo katika vifua vyao kwa walivyopewa (Wahajiri)” na Mwenyezi Mungu kutokana na fadhila na sifa maalumu alizowapa wao tu, ambazo wanazistahiki. Hili linaashiria usalama wa nyoyo zao na kwamba hazina chuki wala uhasidi, na hili pia linaashiria kuwa Muhajirina ni bora kuliko Ansari. Kwa sababu Mwenyezi Mungu aliwataja kwanza kabla yao, na akajulisha kwamba Ansari hawakuona katika nyoyo zao choyo yoyote ya kile walichopewa. Kwa hivyo hilo likaashiria kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwapa kile ambacho hakuwapa Ansari au mtu mwingine yeyote, na kwa sababu walikusanya kati ya usaidizi na kuhama. Na kauli yake: “Bali wanawapendelea kuliko nafsi zao, ingawa wao wenyewe ni wahitaji.” Yaani, katika Sifa za Ansari ambazo kwazo waliwashinda wengine na ambazo kwazo walijitofautisha na wengine ilikuwa ni kupendelea wengine, jambo ambalo ndilo aina kamili zaidi ya ukarimu wa kutoa, nalo ni kupendelea wengine katika mambo ambayo nafsi inapenda kama vile mali na mengineyo, na kuwapa wengine hivyo, pamoja na kwamba mwenye kutoa anavihitaji. Bali hata anapokuwa na dharura kubwa na hitaji kubwa juu yake. Hili haliwezekani isipokuwa kutokana na tabia safi na kumpenda Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kumtanguliza mbele ya kupenda matamanio ya nafsi na ladha zake. Na katika hayo ni kisa cha yule Muanswari ambaye kwa sababu yake aya hii iliteremshwa, pale alipompendelea mgeni wake kwa chakula chake na chakula cha familia yake na watoto wake, na wao wenyewe wakalala njaa. Kupenedelea ni kinyume cha kujipendea. Kwa hivyo, kupendelea ni jambo la kusifiwa, na kujipendea ni jambo la kukashifiwa; kwa sababu ni katika sifa za ubakhili na uchoyo. Mwenye kupewa kupenedelea, basi hakika atakuwa amewekwa mbali na choyo ya nafsi yake. “Na mwenye kuepushwa uchoyo wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufanikiwa.” Kuwekwa mbali na choyo ya nafsi kunajumuisha kukingwa mbali na choyo katika yote aliyoyaamrishwa. Kwani ikiwa mja atalindwa mbali na choyo ya nafsi yake, basi nafsi yake itajiruhusu kufuata maamrisho ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na atayafanya kwa utiifu, kunyenyekea, na kifua wazi katika kuyafanya, na nafsi yake itamruhusu kuacha yale aliyoharamisha Mwenyezi Mungu, hata kama ni mapendwa kwa nafsi yake. Inayaitia na kuyatamani. Na itamruhusu nafsi yake kutoa mali kwa ajili ya njia ya Mwenyezi Mungu na kutafuta radhi zake, na kwa hilo atapata kufaulu na kushinda. Tofauti na yule ambaye hakuzuiliwa mbali na choyo ya nafsi yake. Bali alipewa mtihani wa choyo wa kufanya heri, jambo ambalo ndilo msingi na kiini cha uovu.