Al-Ghaafir
Ini adalah terjemahan Tafsir as-Saʿdī sebagaimana diterbitkan IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca dari halaman-halaman situs itu. Situs itu tidak menyebutkan siapa yang menerjemahkannya maupun edisi cetak mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan ketentuan untuk mengambil teksnya, sehingga hak untuk menampilkannya belum diverifikasi. Belum ada yang membandingkannya dengan buku cetak, dan belum ada ulama yang meninjaunya. Setiap bagian berdiri di samping ayat-ayat yang diulasnya, yaitu teks Al-Qur’an dari Tanzil, ditampilkan sebagaimana adanya di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh situs itu berdiri bersama bagian sebelumnya, dan indeks menyebutkan setiap ayat semacam itu. Sabīl tidak menulis atau menerjemahkan satu pun darinya.
Teks darisaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil 2026-10-22
ٱلَّذِينَ يَحْمِلُونَ ٱلْعَرْشَ وَمَنْ حَوْلَهُۥ يُسَبِّحُونَ بِحَمْدِ رَبِّهِمْ وَيُؤْمِنُونَ بِهِۦ وَيَسْتَغْفِرُونَ لِلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ رَبَّنَا وَسِعْتَ كُلَّ شَىْءٍ رَّحْمَةً وَعِلْمًا فَٱغْفِرْ لِلَّذِينَ تَابُوا۟ وَٱتَّبَعُوا۟ سَبِيلَكَ وَقِهِمْ عَذَابَ ٱلْجَحِيمِ 7
{7} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha juu ya upole wake kamilifu kwa waja wake waumini na sababu za furaha yao ambazo aliwawekea, si wao wanazozitenda, kama vile kuombewa msamaha na malaika walio karibu naye na kuwaombea dua ili watengenee katika dini yao na akhera yao. Hili linajumuisha pia kujulisha kuhusu utukufu wa malaika wabebao kiti chake cha Enzi na wale walio pembezoni mwake, ukaribu wao kwa Mola wao Mlezi na wingi wa ibada zao na kuwanasihi kwa waja wa Mwenyezi Mungu anayapenda, kwa kuwa wanajua kwamba Mwenyezi Mungu anapenda wakifanya hivyo. Akasema: "Wale wanaobeba kiti chake cha Enzi" cha Mwingi wa rehema, ambacho ndicho paa la viumbe na ndicho kitu kikubwa zaidi, kipana zaidi, kilicho kizuri zaidi na kilicho karibu zaidi na Mwenyezi Mungu, ambacho kilienea ardhi, mbingu, na Kursi (mahali ambapo miguu yake inakanyaga). Mwenyezi Mungu aliwakabidhi malaika hawa kukibeba kiti chake kikuu cha enzi. Hapana shaka kuwa wao ni miongoni mwa Malaika wakubwa zaidi na wenye nguvu zaidi. Kuchaguliwa kwao huku na Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kukibeba kiti chake cha enzi na kuwapa kipaumbele katika kuwataja, na kujulisha kuhusu ukaribu wao kwake kunaashiria kuwa wao ndio aina bora zaidi ya Malaika, amani iwe juu yao. Mwenyezi Mungu alisema: "Na wanane juu ya hawa watakuwa wamebeba Kiti cha Enzi cha Mola wako Mlezi," na "wale walio pembezoni mwake" miongoni mwa Malaika walio karibu na Mwenyezi Mungu kwa daraja na ubora, "wanamtakasa Mola wao Mlezi na kumhimidi." Hii ni sifa kwao kwa sababu ya wingi wa kumwabudu kwao Mwenyezi Mungu, hasa kumtakasa na kumhimidi, na matendo mengine yote ya ibada yanayojumuishwa katika kumtakasa Mwenyezi Mungu na kumsifu. "Na wanawaombea msamaha wale walioamini." Haya ni miongoni mwa manufaa mbalimbali ya Imani na fadhila zake nyingi sana; kwamba Malaika ambao hawana dhambi zozote huwaombea msamaha watu wenye imani. Kwa hivyo, Muumini alijisababishia haya kwa sababu ya imani yake. Na kwa vile msamaha una masharti ambayo hauwezi kutimia ila kwayo - kinyume na yale yanayowajia watu wengi katika akili kwamba, kwa kuuomba tu na kuutaka ndiyo mwisho wake kupata msamaha wa dhambi - Mwenyezi Mungu Mtukufu akataja jinsi wanavyowaombea msamaha kwa kutaja mambo ambayo hautimii isipokuwa kwayo, akasema: "Mola wetu Mlezi! Umekienea kila kitu kwa rehema na ujuzi." Elimu yako imekidhibiti kila kitu, wala chochote cha uzito wa chembe hakiwezi kufichikana kwako katika ardhi wala mbinguni, wala kidogo kuliko hicho wala kikubwa, na rehema yako imekienea kila kitu. Ulimwengu wote, wa juu na wa chini, umejaa rehema za Mwenyezi Mungu Mtukufu, na zimewaenea. "Basi wasamehe wale waliotubu" kutokana na ushirikina na maasia, "na wakaifuata Njia yako" kwa kuwafuata Mitume wako kwa kukupwekesha na kukutii, "na waepushe na adhabu ya Jahannamu." Yaani, waepushe na adhabu yenyewe, na waepushe pia visababu vyake.