Al-Ghaafir
Ini adalah terjemahan Tafsir as-Saʿdī sebagaimana diterbitkan IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca dari halaman-halaman situs itu. Situs itu tidak menyebutkan siapa yang menerjemahkannya maupun edisi cetak mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan ketentuan untuk mengambil teksnya, sehingga hak untuk menampilkannya belum diverifikasi. Belum ada yang membandingkannya dengan buku cetak, dan belum ada ulama yang meninjaunya. Setiap bagian berdiri di samping ayat-ayat yang diulasnya, yaitu teks Al-Qur’an dari Tanzil, ditampilkan sebagaimana adanya di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh situs itu berdiri bersama bagian sebelumnya, dan indeks menyebutkan setiap ayat semacam itu. Sabīl tidak menulis atau menerjemahkan satu pun darinya.
Teks darisaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil 2026-10-22
هُوَ ٱلْحَىُّ لَآ إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ فَٱدْعُوهُ مُخْلِصِينَ لَهُ ٱلدِّينَ ۗ ٱلْحَمْدُ لِلَّهِ رَبِّ ٱلْعَـٰلَمِينَ 65
{65} "Yeye ndiye aliye Hai", uhai kamili wenye sifa zake za kidhati ambazo uhai wake hautimii ila kwazo, kama vile kusikia, kuona, uwezo, elimu, usemi na sifa nyinginezo za ukamilifu wake na utukufu wake. "Hapana mungu isipokuwa Yeye", ambaye hapana apasaye kuabudiwa kwa haki ila uso wake Mtukufu. "Basi muabuduni." Hili linajumuisha kumuomba dua ya ibaada na dua ya kutaka kitu fulani "mkimsafishia Dini Yeye" kwa ibada zote na dua, na kufanya matendo kwa ajili ya uso wa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kwani, kilichoamrishwa ni mtu kuwa na Ikhlasi; Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Nao hawakuamrishwa kitu ila wamuabudu Mwenyezi Mungu kwa kumtakasia Dini, wawe waongofu." "Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote," sawa ziwe kwa kauli kama vile viumbe kutamka kwa kumtaja, au kwa vitendo kama vile kumuabudu. Yote haya ni ya Mwenyezi Mungu peke yake. Hana mshirika kwa sababu ya ukamilifu wake katika sifa zake, vitendo vyake na ukamilifu wa neema zake.