Langsung ke konten
Tafsir As-Saadi - Swahili · Yunus
Surah 10

Yunus

Ini adalah terjemahan Tafsir as-Saʿdī sebagaimana diterbitkan IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca dari halaman-halaman situs itu. Situs itu tidak menyebutkan siapa yang menerjemahkannya maupun edisi cetak mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan ketentuan untuk mengambil teksnya, sehingga hak untuk menampilkannya belum diverifikasi. Belum ada yang membandingkannya dengan buku cetak, dan belum ada ulama yang meninjaunya. Setiap bagian berdiri di samping ayat-ayat yang diulasnya, yaitu teks Al-Qur’an dari Tanzil, ditampilkan sebagaimana adanya di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh situs itu berdiri bersama bagian sebelumnya, dan indeks menyebutkan setiap ayat semacam itu. Sabīl tidak menulis atau menerjemahkan satu pun darinya.

Teks darisaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil 2026-10-22

Ayat 64

لَهُمُ ٱلْبُشْرَىٰ فِى ٱلْحَيَوٰةِ ٱلدُّنْيَا وَفِى ٱلْـَٔاخِرَةِ ۚ لَا تَبْدِيلَ لِكَلِمَـٰتِ ٱللَّهِ ۚ ذَٰلِكَ هُوَ ٱلْفَوْزُ ٱلْعَظِيمُ 64

{64} Na "Wao wana bishara njema katika uhai wa dunia na katika Akhera" Ama bishara katika dunia, hiyo ni sifa nzuri na upendo katika nyoyo za Waumini, na ndoto njema, na yale anayoyaona mja miongoni mwa upole wa Mwenyezi Mungu kwake, na kumsahihisha kwake matendo mazuri na tabia nzuri, na kumuondoa kwenye tabia mbaya. Na ama katika akhera, basi ya kwanza yake ni kubashiriwa wakati wa kuchukuliwa roho zao, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu, "Hakika wale waliosema, "Mola wetu Mlezi ni Mwenyezi Mungu! Kisha wakanyooka sawa, hao Malaika huwateremkia wakawaambia: Msihofu, wala msihuzunike. Nanyi pokeeni bishara ya Pepo ambayo mlikuwa mkiahidiwa." Na ndani ya kaburi kuna bishara ya kuridhiwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu na neema ya kudumu. Na katika Akhera kuna bishara kamili ya kuingia katika Mabustani ya neema na kuokoka na adhabu chungu. "Hakuna mabadiliko katika maneno ya Mwenyezi Mungu" bali yale aliyoyaahidi Mwenyezi Mungu, basi hayo ni haki ambayo haiwezi kughairishwa wala kubadilishwa. Kwa sababu, Yeye ndiye Mkweli katika Anayoyasema, ambaye hakuna yeyote anayeweza kupingana Naye katika yale aliyojalia na kuyahukumu. "Huko ndiko kufuzu kukubwa" kwa sababu kunajumuisha wokovu kutokana na kila kinachoepukwa, na ushindi juu ya kila kitafutwacho, kipendwacho. Na alikufungia kufaulu katika hilo kwa sababu, hakuna kufaulu kwa wasiokuwa wenye imani na uchamungu. Na muhtasari wa hilo ni kuwa bishara hii njema inajumuisha kila heri, na malipo ambayo Mwenyezi Mungu ameiwekea katika dunia na akhera kwa sababu ya imani na uchamungu. Na ndiyo maana akaliacha hilo bila ya kulifungia.