Al-Ghaafir
Wannan fassarar tafsirin as-Saʿdī ce, kamar yadda IslamHouse.com ke wallafa ta a saadi.islamenc.com, an karanta ta daga shafukan wannan shafin yanar gizo. Shafin bai faɗi wanda ya fassara ta ba, ko wane bugu da aka buga take bi, kuma bai bayyana sharuɗɗa na ɗaukar rubutunta ba, saboda haka ba a tabbatar da haƙƙin nuna ta ba. Babu wanda ya kwatanta ta da littafin da aka buga, kuma babu malami da ya duba ta. Kowane sashe yana kusa da ayoyin da yake bayani a kansu, waɗanda rubutun Alƙur’ani ne na Tanzil, kamar yadda yake a can; aya da shafin bai ba ta bayani na kanta ba tana tare da sashen da ya gabace ta, kuma jerin yana ambaton kowace irin wannan aya. Sabīl bai rubuta wani abu daga cikinta ba, kuma bai fassara ta ba.
Rubutu dagasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)an ɗauka 2026-10-22
حمٓ 1 تَنزِيلُ ٱلْكِتَـٰبِ مِنَ ٱللَّهِ ٱلْعَزِيزِ ٱلْعَلِيمِ 2 غَافِرِ ٱلذَّنۢبِ وَقَابِلِ ٱلتَّوْبِ شَدِيدِ ٱلْعِقَابِ ذِى ٱلطَّوْلِ ۖ لَآ إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ إِلَيْهِ ٱلْمَصِيرُ 3
{1 - 3} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kuhusu Kitabu chake Kikuu na kwamba kilianzia na kiliteremshwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu, ambaye anafanyiwa uungu, anayeabudiwa kwa sababu ya ukamilifu wake na upekee wake katika vitendo vyake. "Mwenye nguvu" ambaye kwa nguvu zake alikishinda kila kiumbe. "Ajuaye zaidi" kila kitu, "Anayesamehe dhambi" za wafanyao madhambi "na anayepokea toba" za wale wanaotubu, "Mkali wa kuadhibu" wale wanaothubutu kufanya dhambi na hawakutubu. "Mwenye ukarimu" juu ya walimwengu wote. Alipothibitisha yale aliyothibitisha kuhusu ukamilifu wake, na hilo likamlazimu kwamba Yeye pekee ndiye anayepasa kufanyiwa uungu ambaye anakusudiwa peke yake na matendo, akasema: "Hakuna mungu ila Yeye; marejeo ni kwake." Hapa, uhusiano ulipo kwa kutaja kwamba Qur-ani iliteremka kutoka kwa Mwenyezi Mungu, ambaye anasifika kwa sifa hizi ni kwamba sifa hizi zinalazimu kuwepo kwa maana zote zilizomo ndani ya Qur-ani. Kwa maana Qur-ani ima inajulisha kuhusu majina ya Mwenyezi Mungu, sifa zake na vitendo vyake, na haya ni majina, sifa na vitendo. Au ni kujulisha kuhusu ghaibu zilizopita na zijazo, na hayo ni katika mambo ambayo Yule ajuaye zaidi anawafunza waja wake. Au ni kujulisha kuhusu neema zake kubwa, na amri zinazofikisha katika hayo. Hayo yanaonyeshwa na kauli yake: "Mwenye ukarimu." Au ni kujulisha kuhusu adhabu zake kali na maasi yanayozisababisha na kuzilazimu. Haya yanaashiriwa na kauli yake: "Mkali wa kuadhibu" Au ni wito kwa wenye dhambi kutubu, kurudi kwake na kutafuta msamaha. Haya yanaashiriwa na kauli yake: "Anayesamehe dhambi na anayepokea toba, Mkali wa kuadhibu" Au ni kujulisha kwamba Yeye peke yake ndiye anayepasa kufanyiwa uungu na kuabudiwa, na kusimamisha ushahidi wa kiakili na wa kimaandiko juu ya hayo, na kuhimiza juu yake, kukataza na kuabudu kitu chochote kisichokuwa Mwenyezi Mungu, na kusimamisha ushahidi wa kiakili na wa kimaandiko juu ya ubovu wake, na kutishia dhidi yake. Haya yanaashiriwa na kauli yake Mola Mtukufu: "Hakuna mungu ila Yeye." Au ni kujulisha kuhusu hukumu yake ya uadilifu na malipo ya wafanyao wema, na adhabu ya wafanyao maasia. Haya yanaashiriwa na kauli yake: "marejeo ni kwake." Haya yote ndiyo mambo ambayo Qur-ani inajumuisha miongoni mwa matakwa ya juu.