An-Nisaa
Wannan fassarar tafsirin as-Saʿdī ce, kamar yadda IslamHouse.com ke wallafa ta a saadi.islamenc.com, an karanta ta daga shafukan wannan shafin yanar gizo. Shafin bai faɗi wanda ya fassara ta ba, ko wane bugu da aka buga take bi, kuma bai bayyana sharuɗɗa na ɗaukar rubutunta ba, saboda haka ba a tabbatar da haƙƙin nuna ta ba. Babu wanda ya kwatanta ta da littafin da aka buga, kuma babu malami da ya duba ta. Kowane sashe yana kusa da ayoyin da yake bayani a kansu, waɗanda rubutun Alƙur’ani ne na Tanzil, kamar yadda yake a can; aya da shafin bai ba ta bayani na kanta ba tana tare da sashen da ya gabace ta, kuma jerin yana ambaton kowace irin wannan aya. Sabīl bai rubuta wani abu daga cikinta ba, kuma bai fassara ta ba.
Rubutu dagasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)an ɗauka 2026-10-22
مَّن يُطِعِ ٱلرَّسُولَ فَقَدْ أَطَاعَ ٱللَّهَ ۖ وَمَن تَوَلَّىٰ فَمَآ أَرْسَلْنَـٰكَ عَلَيْهِمْ حَفِيظًا 80
80. Yani kila mwenye kumtii Mtume wa Mwenyezi Mungu katika amri zake na makatazo yake, “basi hakika amemtii Mwenyezi Mungu” Mtukufu, kwa sababu haamrishi wala hakatazi isipokuwa kwa amri ya Mwenyezi Mungu, na sheria yake, na wahyi wake, na uteremsho wake. Na katika hilo kuna kumhifadhi Mtume - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake. - Kwa sababu, Mwenyezi Mungu aliamuru atiiwe kabisa. Na lau kuwa hajahifadhiwa na Mwenyezi Mungu katika kila jambo analofikisha kutoka kwa Mwenyezi Mungu, basi hangeamrisha kumtii kabisa, na kulisifu hilo. Na hili ni katika haki za kushirikiana ndani yake. Kwa maana, haki ni tatu: haki ya Mwenyezi Mungu ambayo haiwi ya yeyote miongoni mwa viumbe. Nayo ni kumwabudu Mwenyezi Mungu na kumtaka Yeye, na yanayofuatana na hilo. Na sehemu ambayo ni maalum kwa Mtume. Nayo ni kumuunga mkono, na na kumheshimu, na kumnusuru. Na sehemu ambayo wanashirikiana ndani yake wote. Nayo ni kumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na kuwapenda na kuwatii, kama Mwenyezi Mungu alivyojumuisha kati ya haki hizi katika kauli yake. “Ili mumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na mumuunge mkono, na mumheshimu, na mumtakase asubuhi na jioni.” Basi mwenye kumtii Mtume, basi bila shaka atakuwa amemtii Mwenyezi Mungu, na ana thawabu na heri zilizoekwa juu ya kumtii Mwenyezi Mungu. “Na mwenye kugeuka” kutoka katika kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake, basi yeye kwa hakika hadhuru isipokuwa yeye mwenyewe tu, wala hamdhuru Mwenyezi Mungu kitu. “Basi Sisi hatukukutuma uwe mlinzi juu yao.” Yani mwenye kuyahifadhi matendo yao na hali zao. Bali tulikutuma uwe mfikishaji, mbainishaji na mshauri, na tayari ulikwisha fanya kazi yako, na malipo yako yamekwisha fika kwa Mwenyezi Mungu, sawa waongoke au wasiongoke. Kama alivyosema Yeye Mtukufu, “Basi kumbusha! Hakika, wewe ni Mkumbushaji. Wewe si mwenye kuwatawala,” hadi mwisho wa Aya.