Tsallaka zuwa abin da ke ciki
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Baqara
Sura ta 2

Al-Baqara

Wannan fassarar tafsirin as-Saʿdī ce, kamar yadda IslamHouse.com ke wallafa ta a saadi.islamenc.com, an karanta ta daga shafukan wannan shafin yanar gizo. Shafin bai faɗi wanda ya fassara ta ba, ko wane bugu da aka buga take bi, kuma bai bayyana sharuɗɗa na ɗaukar rubutunta ba, saboda haka ba a tabbatar da haƙƙin nuna ta ba. Babu wanda ya kwatanta ta da littafin da aka buga, kuma babu malami da ya duba ta. Kowane sashe yana kusa da ayoyin da yake bayani a kansu, waɗanda rubutun Alƙur’ani ne na Tanzil, kamar yadda yake a can; aya da shafin bai ba ta bayani na kanta ba tana tare da sashen da ya gabace ta, kuma jerin yana ambaton kowace irin wannan aya. Sabīl bai rubuta wani abu daga cikinta ba, kuma bai fassara ta ba.

Rubutu dagasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)an ɗauka 2026-10-22

Aya ta 283

وَإِن كُنتُمْ عَلَىٰ سَفَرٍ وَلَمْ تَجِدُوا۟ كَاتِبًا فَرِهَـٰنٌ مَّقْبُوضَةٌ ۖ فَإِنْ أَمِنَ بَعْضُكُم بَعْضًا فَلْيُؤَدِّ ٱلَّذِى ٱؤْتُمِنَ أَمَـٰنَتَهُۥ وَلْيَتَّقِ ٱللَّهَ رَبَّهُۥ ۗ وَلَا تَكْتُمُوا۟ ٱلشَّهَـٰدَةَ ۚ وَمَن يَكْتُمْهَا فَإِنَّهُۥٓ ءَاثِمٌ قَلْبُهُۥ ۗ وَٱللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ عَلِيمٌ 283

{283} "Basi yatosha kukabidhiwa rehani " Kwamba ikiwa aliyeweka rehani na aliyepewa rehani watatofautiana katika kiasi cha deni ambalo limewekewa rehani; kwamba kauli sahihi ni kauli ya aliyeweka rehani, mwenye haki. Kwa sababu Mwenyezi Mungu aliifanya rehani kuwa ni dhamana ya kulinda haki yake. Na lau kuwa isingekubaliwa kauli yake katika hilo, basi dhamana isingepatikana ndani yake kwa sababu ya ukosefu wa maandishi na mashahidi. Na miongoni mwake ni kwamba, inaruhusika kuamiliana bila ya dhamana wala mashahidi. Kwa kauli yake, "na mmoja wenu akimwekea amana mwenziwe, basi aliyeaminiwa airudishe amana ya mwenzake." Lakini katika hali hii, anahitaji uchamungu na hofu kwa Mwenyezi Mungu, vinginevyo mwenye haki anahatarisha haki yake. Na kwa sababu hii, Mwenyezi Mungu aliamrisha katika hali hii yule ambaye haki iko juu yake, kumcha Mwenyezi Mungu na kuirudisha amana yake. Na miongoni mwake ni kwamba, unayemkabidhi muamala, basi amemfanyia hisani kubwa na ameridhika na dini yake na uaminifu wake. Basi anamlazimu mno yule ambaye kuna haki juu yake kutekeleza amana yake kwa pande mbili: Kutekeleza haki ya Mwenyezi Mungu na kufuata amri yake. Na kutimiza haki ya mwenzake ambaye aliridhika na uaminifu wake na akamwamini. Na miongoni mwake ni, uharamu wa kuficha ushuhuda. Na kwamba mwenye kuificha moyo wake umetenda dhambi ambayo ndio mfalme wa viungo. Na hilo ni kwa sababu kuificha ni sawa na kutoa ushahidi wa batili na uwongo. Ambao ndani yake kuna kupoteza haki na kuharibika kwa miamala, na dhambi ya kujirudia katika dhima yake na dhima ya yule ambaye haki iko juu yake. Na ama kuifungamanisha rehani na safari pamoja na kwamba inaruhusika nyumbani na safarini, ni kwa sababu ya kulihitaji hilo kwa sababu ya kutokuwepo mwandishi na shahidi. Na alihitimisha Aya hii kwa kusema kuwa Yeye ni Mwenye kujua kila wanachofanya waja wake. (Ili) iwe kama himizo kwao kufanya maamiliano mazuri, na kuwatia hofu kutokana na maamiliano maovu.