Ash-Sharh
This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.
Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22
أَلَمْ نَشْرَحْ لَكَ صَدْرَكَ 1 وَوَضَعْنَا عَنكَ وِزْرَكَ 2 ٱلَّذِىٓ أَنقَضَ ظَهْرَكَ 3 وَرَفَعْنَا لَكَ ذِكْرَكَ 4
{1 - 4} Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema akimkumbusha Mtume wake neema zake: "Hatukukunjulia kifua chako" Kwa kukuteremshia sheria za dini, wito kwa Mwenyezi Mungu, kuwa na maadili mema, kutafuta maisha ya akhera, na kusahihisha mambo ya heri. Kwani hakikuwa chenye dhiki kilichobanika kisichotaka kufuata heri. "Na tukakuondolea mzigo wako" yaani, dhambi zako. "Uliovunja mgongo wako?" Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Ili Mwenyezi Mungu akusamehe makosa yako yaliyotangulia na yajayo" kisha akasema "Na tukakunyanyulia utajo wako?" Yaani, tumeitukuza hadhi yako, na tumekufanya kutajwa kwa sifa nzuri na za hali ya juu ambazo hakuna hata mmoja miongoni mwa viumbe aliyewahi kuzifikia. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu hatajwi, isipokuwa Mtume wake – rehema na amani zimshukie – atatajwa pamoja naye. Kama ilivyo katika kuingia katika Uislamu, katika adhana, kukimu swala, khutba mbalimbali... na mambo mengineyo miongoni mwa mambo ambayo Mwenyezi Mungu ameuinua utajo wa Mtume wake Muhammad -rehema na amani zimshukie - naye anao katika nyoyo za umma wake upendo, heshima na taadhima ambazo hakuna mtu mwingine yeyote anazo baada ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kwa hivyo Mwenyezi Mungu amlipe kwa sababu ya umma wake bora zaidi ya anavyowezakumlipa Nabii kwa sababu ya umma wake.