At-Tawba
This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.
Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ لَا تَتَّخِذُوٓا۟ ءَابَآءَكُمْ وَإِخْوَٰنَكُمْ أَوْلِيَآءَ إِنِ ٱسْتَحَبُّوا۟ ٱلْكُفْرَ عَلَى ٱلْإِيمَـٰنِ ۚ وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَأُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلظَّـٰلِمُونَ 23
{23} Yeye Mtukufu anasema: "Enyi mlioamini!" tendeni kulingana na matakwa ya imani yenu, kwa kuwafanya marafiki wale walioamini, na kuwafanyia uadui wale ambao hawakuamini, na "Msiwafanye baba zenu na ndugu zenu" ambao ndio watu wa karibu zaidi kwenu, na wengineo kwa njia ya kustahili na kufaa zaidi, basi msiwafanye kuwa "marafiki walinzi wenu ikiwa wanapendelea." Yaani, ikiwa watachagua kwa namna ya kuridhia na kupenda, "ukafiri kuliko Imani. Na mwenye kuwafanya marafiki walinzi miongoni mwenu, basi hao ndio madhalimu;" kwa sababu, walimuasi Mwenyezi Mungu kwa ujasiri, na wakawafanya maadui wa Mwenyezi Mungu kuwa marafiki walinzi. Na msingi wa Al-Wilaaya ni upendo na nusura. Na hilo ni kwamba kuwafanya kuwa marafiki walinzi kunalazimu kutanguliza utiifu kwao mbele ya utiifu kwa Mwenyezi Mungu na upendo wao mbele ya upendo wa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake.