Skip to content
Tafsir As-Saadi - Swahili · At-Tawba
Sūrah 9

At-Tawba

This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.

Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22

Verses 1–2

بَرَآءَةٌ مِّنَ ٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦٓ إِلَى ٱلَّذِينَ عَـٰهَدتُّم مِّنَ ٱلْمُشْرِكِينَ 1 فَسِيحُوا۟ فِى ٱلْأَرْضِ أَرْبَعَةَ أَشْهُرٍ وَٱعْلَمُوٓا۟ أَنَّكُمْ غَيْرُ مُعْجِزِى ٱللَّهِ ۙ وَأَنَّ ٱللَّهَ مُخْزِى ٱلْكَـٰفِرِينَ 2

[1-2] Yaani, huku ni "kujiweka mbali kutokako kwa Mwenyezi Mungu" na kutokako kwa "Mtume wake" kuwaendea washirikina wote walioahidiana nanyi (Waumini), kwamba wana miezi minne ya kutembea katika ardhi kwa hiari yao, wakiwa salama kutokana na Waumini. Na baada ya miezi minne hii, hawatakuwa na ahadi yoyote wala agano. Na hili ni yule aliyekuwa na agano ambalo halikufungiwa katika muda maalumu, au ambalo halikuwekewa muda wa miezi minne au chini. Ama yule aliyekuwa na agano lililowekewa muda wa zaidi ya miezi minne, basi italazimu atimiziwe agano lake ikiwa hatahofiwa kufanya uhaini na wala hakuanza yeye kulivunja agano hilo. Kisha akawaonya wale waliofanya agano katika kipindi cha agano lao kwamba hata kama watakuwa salama, wao kwa hakika hawatamshinda Mwenyezi Mungu wala hawatafanya awakose. Na kwamba mwenye kuendelea miongoni mwao na ushirikina wake, basi hakuna budi atamhizi. Kwa hivyo hili likawa miongoni mwa yale yanayowavutia kuingia katika Uislamu isipokuwa yule aliyekaidi, na akasisitiza, na hakujali ahadi mbaya hii ya Mwenyezi Mungu.