Al-Qalam
This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.
Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22
إِنَّ لِلْمُتَّقِينَ عِندَ رَبِّهِمْ جَنَّـٰتِ ٱلنَّعِيمِ 34 أَفَنَجْعَلُ ٱلْمُسْلِمِينَ كَٱلْمُجْرِمِينَ 35 مَا لَكُمْ كَيْفَ تَحْكُمُونَ 36 أَمْ لَكُمْ كِتَـٰبٌ فِيهِ تَدْرُسُونَ 37 إِنَّ لَكُمْ فِيهِ لَمَا تَخَيَّرُونَ 38 أَمْ لَكُمْ أَيْمَـٰنٌ عَلَيْنَا بَـٰلِغَةٌ إِلَىٰ يَوْمِ ٱلْقِيَـٰمَةِ ۙ إِنَّ لَكُمْ لَمَا تَحْكُمُونَ 39 سَلْهُمْ أَيُّهُم بِذَٰلِكَ زَعِيمٌ 40 أَمْ لَهُمْ شُرَكَآءُ فَلْيَأْتُوا۟ بِشُرَكَآئِهِمْ إِن كَانُوا۟ صَـٰدِقِينَ 41
{34 - 41} Mwenyezi Mungu Mtukufu anatuambia kile alichowaandalia wacha Mungu waliojiepusha na ukafiri na maasi, miongoni mwa aina mbalimbali za furaha na maisha salama mno karibu na Mkarimu zaidi ya wakarimu wote, na kwamba hekima yake Mtukufu haifailii awafanye wacha Mungu, watiifu kwa Mola wao Mlezi, wanaotekeleza amri zake, na wanafuata yale yanayomridhisha, kama wahalifu waliozama katika kumuasi, na kuzikufuru Aya zake, na kuwapinga Mitume wake, na kupigana na vipenzi wake, na kwamba wanaodhani kwamba yeye atawafanya sawa katika malipo, basi hakika amehukumu vibaya, na kwamba hukumu yake hiyo ni [hukumu] batili na maoni mabovu, na kwamba wahalifu wanapokidai hivyo, wao huwa hawana msingi wowote wa kushikilia, si kitabu ambacho wanakidurusu na kusoma ndani yake kwamba wao ni miongoni mwa watu wa Peponi, na kwamba watapata yale waliyoyaomba na waliyoyachagua, na pia hawana ahadi na kiapo kwa Mwenyezi Mungu vinavyofika Siku ya Kiyama kwamba watapata yale wanayohukumu, na hawana washirika na wasaidizi watakaowasaidia kufikia yale wanayoyataka. Ikiwa wanao washirika na wasaidizi, basi wawalete ikiwa ni wakweli. Lakini kama inavyojulikana kuwa kwamba yote haya hayapo. Hawana kitabu, wala hawana ahadi kwa Mwenyezi Mungu kuhusiana na kuokoka kwao, wala hawana washirika wa kuwasaidia. Kwa hivyo ikajulikana kwamba madai yao hayo ni batili na mabovu. Na kauli yake: “Waulize: Ni nani miongoni mwao dhamini wa haya" ambayo yameshabainika ubatili wake? Kwani, haiwezekani kwa mtu yeyote kuyaweza wala kuwa mdhamini wake.