Skip to content
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Qalam
Sūrah 68

Al-Qalam

This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.

Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22

Verse 15

إِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِ ءَايَـٰتُنَا قَالَ أَسَـٰطِيرُ ٱلْأَوَّلِينَ 15

{15} Na Aya hizi hata kama ziliteremshwa kuhusiana na baadhi ya washirikina, kama vile Al-Walid bin Al-Mughirah au wengineo, kwa sababu ya yale aliyosema juu yake: "Ati kwa kuwa ana mali na watoto! Anaposomewa Aya zetu, husema: Hizi ni simulizi za uwongo za watu wa zamani!" Yaani, kwa sababu ya mali yake nyingi na watoto wake, alikuvuka mipaka na akaifanyia kiburi haki na akaikataa ilipomjia na akaifanya kuwa miongoni mwa ngano za watu wa kale zinazoweza kuwa za kweli au za uongo, lakini pamoja na hili, aya hii ni ya jumla kwa kila mtu ambaye ana maelezo haya. Kwa sababu Qur-ani imeteremshwa kwa ajili ya kuwaongoa viumbe wote, na inajumuisha wa mwanzo wa Umma huu na wa mwisho wake, na pengine baadhi ya Aya ziliteremshwa kwa sababu ya mtu fulani, ili ibainike vyema kanuni fulani ya jumla, na ili kwa hilo ijulikane mifano ya kina ambayo inajumuishwa katika masuala ya jumla.