Skip to content
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Mumtahana
Sūrah 60

Al-Mumtahana

This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.

Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22

Verse 1

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ لَا تَتَّخِذُوا۟ عَدُوِّى وَعَدُوَّكُمْ أَوْلِيَآءَ تُلْقُونَ إِلَيْهِم بِٱلْمَوَدَّةِ وَقَدْ كَفَرُوا۟ بِمَا جَآءَكُم مِّنَ ٱلْحَقِّ يُخْرِجُونَ ٱلرَّسُولَ وَإِيَّاكُمْ ۙ أَن تُؤْمِنُوا۟ بِٱللَّهِ رَبِّكُمْ إِن كُنتُمْ خَرَجْتُمْ جِهَـٰدًا فِى سَبِيلِى وَٱبْتِغَآءَ مَرْضَاتِى ۚ تُسِرُّونَ إِلَيْهِم بِٱلْمَوَدَّةِ وَأَنَا۠ أَعْلَمُ بِمَآ أَخْفَيْتُمْ وَمَآ أَعْلَنتُمْ ۚ وَمَن يَفْعَلْهُ مِنكُمْ فَقَدْ ضَلَّ سَوَآءَ ٱلسَّبِيلِ 1

Wafasiri wengi, Mwenyezi Mungu awarehemu, walitaja kuwa sababu ya kuteremshwa aya hizi tukufu ni kuhusiana na kisa cha Hatib bin Abi Balta’a, wakati Nabii – rehema na amani zimshukie – alipotaka kwenda vita vya utekaji Makka, Hatib aliwaandikia washirikina wa kutoka kwa watu wa Makka akiwajulisha kuhusu kundoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – akiwajia; ili apate wa kumsaidia kwa hilo miongoni mwao, siyo kwa sababu ya kuwa na shaka wala unafiki. Aliituma pamoja na mwanamke fulani, lakini Nabii – rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie – akajulishwa juu yake, kwa hivyo akatuma atafutwe mwanamke huyo kabla hajafika huko. Basi wakaichukua barua hiyo kutoka kwake, na akamlaumu Hatib, naye akaomba radhi kwa udhuru ambao Mtume – rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie – aliukubali. Aya hizi zina makatazo makali ya kuwaunga mkono makafiri, wawe ni washirikina au wengineo, na kuwapa mapenzi, na kwamba jambo hilo ni kinyume na imani na ni kinyume na dini ya Ibrahim, mwandani wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani ziwe juu yake, na ni kinyume na akili, ambayo inahitaji kuchukua tahadhari kamili dhidi ya adui ambaye haachi chochote katika juhudi zake za kufanya uadui na kuchukua fursa ya kufikisha madhara kwa adui yake.

{1} Akasema Mwenyezi Mungu: “Enyi mlioamini;” yaani, tenda kwa mujibu wa imani yenu, ya kuwafanya vipenzi wale walioamini, na kuwafanyia uadui wale wanaoifanyia uadui. Kwani yeye ni adui wa Mwenyezi Mungu na ni adui wa Waumini. Basi “Msiwafanye adui zangu na adui zenu kuwa marafiki mkiwapa mapenzi.” Yaani, msikimbilie kuwapenda na kujitahidi kufanya visababu vyake. Kwani ikiwa mapenzi kama hayo yakitokea, basi yatafuatwa na usaidizi na kushirikiana mno, basi mja akawa ametoka katika Imani na akawa miongoni mwa watu makafiri [na kujitenga na watu wa imani]. Mtu huyu anayemchukulia kafiri kuwa rafiki mlinzi msaidizi pia hana uungwana. Vipi anamfanya rafiki mlinzi msaidizi yule ambaye ndiye adui yake kuliko maadui wote, ambaye hamtakii isipokuwa uovu, na anakwenda kinyume na Mola wake Mlezi na rafiki mlinzi msaidizi wake huyu ambaye anamtakia heri, na anamwamrisha na kumhimiza juu yake? Na pia katika yale yanayomwita Muumini kuwafanyia uadui makafiri ni kwamba wamekufuru haki iliyowajia Waumini, na hakuna kubwa zaidi ya kuhalifu huku na upinzani huu. Kwani walikufuru msingi wa dini yenu, na wakadai kwamba nyinyi mmepotea na hamko kwenye uwongofu. Lakini hali halisi ni kwamba wao waliikufuru haki isiyo na shaka yoyote wala kusitasita. Na mwenye kuikataa haki, basi haiwezekani awe na ushahidi au hoja inayoonyesha usahihi wa kauli yake. Bali kujua tu haki, kunaonyesha ubatili na uharibifu wa kauli ya aliyeikataa. Miongoni mwa uadui wao mkubwa zaidi ni kwamba “walimfukuza Mtume na nyinyi” enyi Waumini, na kukutoeni katika nyumba zenu, na kukufukuzeni kutoka katika nchi yenu hali ya kuwa hamkuwakosea lolote ndo wafanye hivyo, isipokuwa dhambi mnamwamini Mola wenu Mlezi, “Mwenyezi Mungu, Mola wenu Mlezi.” Ambye ni lazima kwa viumbe vyote kumuabudu, Kwa sababu Yeye ndiye aliyewalea, na akawapa neema za dhahiri na zilizofichika [naye ni Mwenyezi Mungu Mtukufu]. basi walipolipa mgongo jambo hili ambalo ndilo faradhi kubwa zaidi, nany mkalitekeleza, wakufanyieni uadui na kukutoeni majumbani mwenu. Basi ni dini gani, uungwana gani, na akili gani inabakiapamoja na mja ikiwa atawafanya makafiri kuwa vipenzi wasaidizi, wale ambao haya ndiyo maelezo yao katika kila wakati au mahali, na wala hakuna kinachowazuilia kufanya hivyo isipokuwa hofu tu au kizuizi chenye nguvu. “Mnapotoka kwa ajili ya Jihadi katika Njia yangu na kutafuta radhi yangu.“ Yaani: Ikiwa nia yenu ilikuwa kwenda kufanya hijadi katika njia ye Mwenyezi Mungu, ili kuinua juu neno la Mwenyezi Mungu na kutafuta radhi zake, basi tendeni kulingana na hili, kwa kufanya urafiki wendani na vipenzi wa Mwenyezi Mungu na kuwa na kuwafanyia uadui adui zake. Hii hakika ni miongoni mwa jihadi kubwa zaidi katika njia yake, na ni katika mambo mkubwa zaidi ambayo kwayo wale wanaojiweka karibu wanajiweka karibu na Mwenyezi Mungu na kutafuta kwayo radhi zake. “Mnafanya urafiki nao kwa siri, na Mimi nayajua mnayoyaficha na mnayodhihirisha.” Yaani, vipi mnafanya urafiki kwa siri ya makafiri na hali mnajua kwamba Mwenyezi Mungu anayajua mnayoyaficha na mnayoyadhihirisha? Hata ikiwa hilo likafichika kwa Waumini, halifichiki kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na atawalipa waja wake kwa yale anayoyajua kwao; mema na mabaya. “Na mwenye kufanya hayo kati yenu.” Yaani, kufanya urafiki wandani na kuwaunga mkono makafiri baada ya Mwenyezi Mungu kuwahadharisha nalo “basi ameipotea njia ya sawa;” kwa sababu yeye alishika njia iliyo kinyume na sheria, akili na uungwana.