Al-An'aam
This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.
Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22
إِنَّ ٱللَّهَ فَالِقُ ٱلْحَبِّ وَٱلنَّوَىٰ ۖ يُخْرِجُ ٱلْحَىَّ مِنَ ٱلْمَيِّتِ وَمُخْرِجُ ٱلْمَيِّتِ مِنَ ٱلْحَىِّ ۚ ذَٰلِكُمُ ٱللَّهُ ۖ فَأَنَّىٰ تُؤْفَكُونَ 95
{95} Yeye Mtukufu anajulisha kuhusu ukamilifu Wake, na ukubwa wa mamlaka Yake, na nguvu ya uwezo Wake, na upana wa rehema Yake, na ujumla wa ukarimu Wake, na ukubwa wa utunzaji Wake kwa viumbe Vyake. Akasema, "Hakika Mwenyezi Mungu ndiye mpasuaji nafaka," hili linajumuisha nafaka zote ambazo watu huzipanda, na zile ambazo hawazipandi. Kama vile zile nafaka ambazo Mwenyezi Mungu huzitawanya katika nyika na porini, kisha anapasua nafaka kutokana na mazao na mimea ya kila aina zake, sura zake, na manufaa yake. Na hupasua mbegu kutoka katika miti kame vile mitende, na matunda na isiyokuwa hiyo. Kwa hivyo, wananufaika wanadamu, na mifugo, na wanyama, na wanakula katika vile alivyovipasua Mwenyezi Mungu miongoni mwa nafaka na mbegu, na wanavila na wananufaika na kila aina ya manufaa aliyoyaweka Mwenyezi Mungu katika hivyo. Na Mwenyezi Mungu anawonyesha katika wema wake na ihsani yake yale ambayo huangaza akili na kuzishangaza wanaume wenye nguvu, na huwaonyesha katika ufundi wake wa ajabu na ukamilifu wa hekima yake ambayo kwayo wanamjua na wanampwekesha, na wanajua kuwa Yeye ndiye Haki, na kwamba kumuabudu asiyekuwa Yeye ni batili. "Humtoa aliye hai kutokana na maiti," kama vile anavyotoa mnyama kutoka katika manii, na kifaranga kutoka katika yai, na nafaka na kokwa kutoka katika mimea na miti. "Mwenye kumtoa maiti," naye ni yule ambaye hamei wala hana roho "kutokana na aliye hai;" kama vile anavyotoa kokwa na nafaka kutoka katika miti na mazao. Na anatoa mayai kutoka katika ndege na kadhalika. "Huyo" ambaye alifanya aliyoyafanya, na akawa peke yake katika kuumba vitu hivi, na kuviendesha ndiye "Mwenyezi Mungu" Mola wenu Mlezi. Yaani, Yeye ndiye mwenye uungu na ibada juu ya viumbe vyake vyote. Na ndiye aliyewalea walimwengu wote kwa neema zake, na akawalisha kwa ukarimu wake. "Basi vipi mnadanganywa?" Yaani, vipi mnageuzwa, na mnakataa kumwabudu Yule ambaye mambo yake ni hivi, na mkamuabudu yule asiyeimilikia nafsi yake manufaa yoyote, wala madhara, wala kifo, wala uhai, wala ufufuo?