Al-Mujaadila
This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.
Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22
لَّا تَجِدُ قَوْمًا يُؤْمِنُونَ بِٱللَّهِ وَٱلْيَوْمِ ٱلْـَٔاخِرِ يُوَآدُّونَ مَنْ حَآدَّ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ وَلَوْ كَانُوٓا۟ ءَابَآءَهُمْ أَوْ أَبْنَآءَهُمْ أَوْ إِخْوَٰنَهُمْ أَوْ عَشِيرَتَهُمْ ۚ أُو۟لَـٰٓئِكَ كَتَبَ فِى قُلُوبِهِمُ ٱلْإِيمَـٰنَ وَأَيَّدَهُم بِرُوحٍ مِّنْهُ ۖ وَيُدْخِلُهُمْ جَنَّـٰتٍ تَجْرِى مِن تَحْتِهَا ٱلْأَنْهَـٰرُ خَـٰلِدِينَ فِيهَا ۚ رَضِىَ ٱللَّهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا۟ عَنْهُ ۚ أُو۟لَـٰٓئِكَ حِزْبُ ٱللَّهِ ۚ أَلَآ إِنَّ حِزْبَ ٱللَّهِ هُمُ ٱلْمُفْلِحُونَ 22
{22} Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: “Huwakuti watu wanaomuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho kuwa wanawapenda wanaompinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake.” Yaani, haya na haya hayajumuiki pamoja. Kwa hivyo mja hawezi kuwa ni mwenye kumuamini kihakika Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho isipokuwa atatenda kulingana na matakwa ya imani yake hiyo na mahitaji yake kama vile kumpenda na kumfanya wendani yule ambaye alimwamini, na kuchukia yule ambaye hakufanya hivyo na kumfanyia uadui, hata kama yeye ndiye mtu wa karibu zaidi naye. Hii ndiyo imani ya kweli, ambayo yamepatikana matunda yake na makusudio wake. Na wanaosifika kwa sifa hizi ndio ambao Mwenyezi Mungu “ameandika katika nyoyo zao Imani” akaichora humo, akaiimarisha, akaipanda kupanda ambako haitikisiki wala haiathiriwi fikira potofu wala dhana zozote. Nao ndio wale ambao Mwenyezi Mungu amewapa nguvu “kwa Roho itokayo kwake” yaani kwa wahyi wake, msaada wake wa kimungu, msaada wake, wema wake ya kimungu, nao ndio wenye maisha mema katika nyumba hii, na wana mabustani ya neema katika nyumba ya kubakia, ambayo ndani yake kuna kila kitu ambacho nafsi zinatamani na macho yanafurahia na kuchagua, na wanayo neema iliyo bora zaidi na kubwa zaidi, ambayo ni kwamba Mwenyezi Mungu atawapa radhi yake, na wala hatawakasirikia abadani, nao watamridhia Mola wao Mlezi kwa yale atakayowapa miongoni mwa kila aina ya mambo matukufu, na malipo mazuri mengi, na vipawa teletele, na vyeo vya juu, kiasi kwamba hawataona juu ya yale aliyowapa Mola wao lengo lingine wala mwisho wowote baada yake. Na ama mwenye kudai kwamba anamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, lakini pamoja na hayo, anawapenda maadui wa Mwenyezi Mungu, na kumpenda mwenye kuiacha imani nyuma ya mgongo wake. Hakika hii ni imani ya kujidai tu ambayo haina uhakika wowote. Kwa maana kila jambo ni lazima liwe na ushahidi wa kulisadikisha. Lakini kudai tu hakufai kitu chochote, wala mwenye madai hayo hasadikiwi, na sifa njema ni za Mwenyezi Mungu.