Al-Waaqia
This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.
Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22
أَفَرَءَيْتُم مَّا تَحْرُثُونَ 63 ءَأَنتُمْ تَزْرَعُونَهُۥٓ أَمْ نَحْنُ ٱلزَّٰرِعُونَ 64 لَوْ نَشَآءُ لَجَعَلْنَـٰهُ حُطَـٰمًا فَظَلْتُمْ تَفَكَّهُونَ 65 إِنَّا لَمُغْرَمُونَ 66 بَلْ نَحْنُ مَحْرُومُونَ 67
{63 - 67} Hii ni neema itokayo kwake juu ya waja wake, ambayo kwayo anawaita wampwekeshe, wamwabudu, na wamgeukie yeye. Ambapo aliwaneemesha kwa yale aliyowarahisishia katika suala la kulima mazao na matunda, kisha vinatoka humo chakula, riziki, na matunda ambayo ni miongoni mwa mahitaji yao ya lazima, na masilahi ambayo hawawezi kuyahesabu wakayadhibiti, pamoja na kwamba hawawezi kushukuru hayo na kutimizia haki yake ya sawasawa, basi akawafanya kukiri neema yake hii akasema: "Je, ni nyinyi mnayoyaotesha au ni Sisi ndio wenye kuotesha?" Yaani, je, nyinyi ndio mliiotesha mmea hii kutoka ardhini? Au nyinyi ndio mlioikuza? Au nyinyi ndio mliotoa masuke yake na matunda yake mpaka yakavunwa kama nafaka na matunda yaliyoiva? Au ni Mwenyezi Mungu peke yake ndiye aliyefanya haya na akawapa hivyo kama neema, nami kikubwa mnachofanya tu ni kulima ardhi, kuipasua, na kupanda humo mbegu, kisha huwa hamjui ni kinachotokea baada ya hayo, wala hata hamna uwezo wa kufanya zaidi ya hayo? Hata hivyo; akawatanabahisha kwamba shamba hilo liko kwenye hatari, lau si kutokana na ulinzi wa Mwenyezi Mungu na kuliweka liwe ni lenye kusalia ili liwe ni la usaidizi kwenu na starehe kwa muda. Akasema: " Tungelitaka, tungeliyafanya." Yaani, mazao yaliyolimwa humo na matunda yaliyo ndani yake "yakawa mapepe" yasiyokuwa na manufaa wala riziki, "mkabaki" kwa sababu ya kuyafanywa kuwa mapepe baada ya kutaabika kwenu ndani yake, na kutumia gharama nyingi humo, "mnastaajabu" na kujutia sana yaliyokusibuni, kwa hivyo hilo likaondoa furaha yenu, mkawa mnasema: "Hakika sisi tumegharimika" kwa balaa hii iliyotupata ikatuangamiza. Kisha baada ya hayo ndiyo mtajua mlikotoka wapi, na kwa sababu gani mliteswa? Basi mkasema: "Bali sisi tumenyimwa!" Basi msifuni Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kuwa aliwapandia hayo, kisha akayahifadhi na kuyakamilisha kwa ajili yenu, na wala hakuyatumia balaa ambayo kwayo mngenyimwa manufaa na heri yake.