Al-Qamar
This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.
Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22
إِنَّ ٱلْمُتَّقِينَ فِى جَنَّـٰتٍ وَنَهَرٍ 54 فِى مَقْعَدِ صِدْقٍ عِندَ مَلِيكٍ مُّقْتَدِرٍۭ 55
{54 - 55} "Hakika wacha Mungu" waliokuwa wakifanya maamrisho yake na kuacha makatazo yake, wale waliojiepusha na ushirikina na madhambi makubwa na madogo "watakuwa katika Mabustani na mito" yenye neema. Ambazo ndani yake kuna yale ambayo jicho halijawahi kuyaona, wala sikio halijawahi kuyasikia, wala moyo wa mwanadamu yeyote haujawahi kuyafikiria. Na ndani yake pia kuna miti yenye majani mabichi na matunda, na mito inayotiririka, na makasri yaliyoinuka juu, na majumba mazuri mazuri, na vyakula na vinywaji vitamu, mahurulaini wazuri, na makonde yenye urembo Peponi, na radhi za Mfalme, Mlipaji, na kufaulu kuwa karibu naye, na ndiyo maana akasema: "Katika mahali pa kukalia pa haki kwa Mfalme Mwenye uwezo." Basi hata usiulize baada ya haya yale atakayowapa Mola wao Mlezi katika utukufu wake na utoaji wake kwa wingi, na kuwazidishia wema wake na neema yake. Mwenyezi Mungu atufanye miongoni mwao, wala asitunyime heri aliyo nayo kwa ubaya wa yale tuliyo nayo.
Imekamilika tafsiri ya Sura hii, na sifa njema ni za Mwenyezi Mungu.