Skip to content
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Qamar
Sūrah 54

Al-Qamar

This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.

Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22

Verse 43

أَكُفَّارُكُمْ خَيْرٌ مِّنْ أُو۟لَـٰٓئِكُمْ أَمْ لَكُم بَرَآءَةٌ فِى ٱلزُّبُرِ 43

{43} Malengo ya kutaja hadithi hizi ni kuwaonya watu na wale waliomkadhibisha Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - na ndiyo maana akasema: "Je, makafiri wenu ni bora kuliko hao?" Yaani, je, hawa waliomkanusha Mitume bora zaidi ni bora kuliko wale waliokanusha ambao Mwenyezi Mungu alitaja maangamizo yao na yaliyowasibu? Ikiwa hawa ni bora kuliko wale; basi wataweza kuokoka kutokana na adhabu na hawatakumbwa na yale yaliyowapata watu wale waovu. Lakini sivyo ilivyo. Kwani ikiwa hawa si wabaya kuliko wale, basi wao si bora kuliko wale. "au yameandikwa vitabuni kuwa nyinyi hamtiwi makosani?" Yaani, au je, Mwenyezi Mungu alikupeni ahadi na agano katika vitabu alivyoteremsha kwa Manabii, kwa hivyo mnaamini kwamba nyinyi ndio mtakaofaulu kutokana na habari alizowapa Mwenyezi Mungu na ahadi yake? Hili si jambo la kweli. Bali hata haliwezekani, kiakili na kisheria, kwamba waliandikiwa kutotiwa kwao makosani katika vitabu vya kimungu vinavyojumuisha uadilifu na hekima. Basi siyo katika hekima kuwaokoa watu kama hawa, wakaidi, wanaomkadhibisha Mitume bora zaidi na mtukufu zaidi wao kwa Mwenyezi Mungu.