Al-Maaida
This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.
Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ لَا تَقْتُلُوا۟ ٱلصَّيْدَ وَأَنتُمْ حُرُمٌ ۚ وَمَن قَتَلَهُۥ مِنكُم مُّتَعَمِّدًا فَجَزَآءٌ مِّثْلُ مَا قَتَلَ مِنَ ٱلنَّعَمِ يَحْكُمُ بِهِۦ ذَوَا عَدْلٍ مِّنكُمْ هَدْيًۢا بَـٰلِغَ ٱلْكَعْبَةِ أَوْ كَفَّـٰرَةٌ طَعَامُ مَسَـٰكِينَ أَوْ عَدْلُ ذَٰلِكَ صِيَامًا لِّيَذُوقَ وَبَالَ أَمْرِهِۦ ۗ عَفَا ٱللَّهُ عَمَّا سَلَفَ ۚ وَمَنْ عَادَ فَيَنتَقِمُ ٱللَّهُ مِنْهُ ۗ وَٱللَّهُ عَزِيزٌ ذُو ٱنتِقَامٍ 95
{95} Kisha akakataza waziwazi kumuua windo katika hali ya ihram, kwa hivyo akasema; "Enyi mlioamini! Msiwaue mawindo hali ya kuwa mko katika Ihram (ya Hijja au 'Umra);" yaani, mkiwa mmehirimia Hijja na 'Umra. Na katazo hili la kumuua linajumuisha katazo dhidi ya vitangulizi vya kuua, na kushiriki katika kuua, na kumuashiria, na kusaidia katika kumuua, hadi katika ukamilifu wa hilo ni kwamba anamkataza mtu aliye katika ihramu kula kilichoulia au kuwindwa kwa ajili yake. Na yote haya ni kuitukuza ibada hii kubwa. Kwamba, ni kwa aliye katika Ihram kuua na kuwinda yale yaliyokuwa halali kwake kabla ya kuingia katika ihram. Na kauli yake, "Na miongoni mwenu atakayemuuwa makusudi;" yaani, aliyemuua windo kwa kukusudia, {basi} ni juu yake "malipo yatakayokuwa kuchinja kilicho sawa na alichokiua, katika mifugo." Yaani, ngamia au ng'ombe au kondoo. Na kinaangaliwa kitu kinachofanana na hicho, basi inakuwa wajibu kwake mfano wake, amchinje na amtoe kama sadaka. Na mazingatio yatakuwa kwa kufanana; "kama wanavyohukumu hivyo waadilifu wawili miongoni mwenu. Yaani, watu wawili waadilifu wanaojua kuhukumu na namna ya mfanano. Kama walivyofanya Maswahabah, Mwenyezi Mungu awe radhi nao; ambapo walihukumu kwamba njiwa afidiwe kwa kondoo, na mbuni kwa ngamia, na kwa ng'ombe katika ng'ombe wa mwitu kwa kila aina zake. Na vivyo hivyo kila kitu kinachofanana na kitu kingine miongoni mwa mifugo, basi kitafidiwa kwa mfano wake. Na ikiwa hakifanani na chochote, basi kitafidiwa kwa thamani yake, kama ilivyo kanuni katika vitu vilivyoharibika. Na dhabihu huyu lazima awe "Mnyama anayepelekwa kwenye Al-Kaaba; yaani, achinjiwe katika eneo takatifu. "Au kutoa kafara kwa kuwalisha masikini; yaani, kafara ya adhabu ya hilo ni kuwalisha masikini. Yaani, akifanye kinachotoshana na mfano wake katika mifugo kiwe chakula atakacholisha kwacho masikini. Wengi wa wanachuoni walisema, malipo hayo yanapimwa, kisha kinanunuliwa chakula kwa thamani yake, kisha kila masikini analishwa Mudd ya ngano au nusu Swaa katika vinginevyo. "Au badala ya hayo;" yaani, chakula hicho, "ni kufunga;" yaani, afunge badala ya kulisha kila masikini kwa siku moja; "ili aonje" kwa kusababishwa na malipo haya yaliyotajwa ubaya wa jambo lake hili. Na atakayefanya tena baada ya hayo, basi Mwenyezi Mungu atamuadhibu vikali. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye nguvu, na Mwenye kuadhibu vikali Na Mwenyezi Mungu alitaja hasa aliyemuua windo kwa kukusudia pamoja na kwamba adhabu inamhusu mwenye kukusudia na aliyefanya kwa kukosea. Kama ilivyo kanuni ya kisheria; kwamba, mwenye kuharibu nafsi na mali vilivyoharamishwa, anavidhamini kwa hali yoyote ile, ikiwa kuharibu kwake ni bila ya haki. Kwa sababu Mwenyezi Mungu aliwekea hilo malipo na adhabu, na kisasi. Na hili ni kwa aliyefanya kwa makusudi. Ama mwenye kufanya kwa kukosea,basi yeye hana adhabu, yeye ana malipo tu . (Hii ndiyo kauli ya wanachuoni walio wengi, lakini lililo sahihi ni lile ambalo Aya iliyasema waziwazi kwamba hakuna malipo kwa yule ambaye hakukusudia, kama vile hakuna adhabu juu yake.)