Al-Maaida
This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.
Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22
وَكَيْفَ يُحَكِّمُونَكَ وَعِندَهُمُ ٱلتَّوْرَىٰةُ فِيهَا حُكْمُ ٱللَّهِ ثُمَّ يَتَوَلَّوْنَ مِنۢ بَعْدِ ذَٰلِكَ ۚ وَمَآ أُو۟لَـٰٓئِكَ بِٱلْمُؤْمِنِينَ 43
{43} Kisha akasema akiwashangaa, "Na vipi wanakufanya kuwa hakimu wao ilhali wanayo Taurati yenye hukumu za Mwenyezi Mungu ndani yake? Kisha baada ya hayo wanageuka. Na hao si Waumini." Kwa maana kama wangekuwa waumini, wafanyao kwa yale ambayo imani yao inataka na kuwajibisha, basi hawangejiepusha na hukumu ya Mwenyezi Mungu ambayo iko katika Taurati ambayo wanayo mikononi mwao, isipokuwa ili wapate kwako kile kinachoafikiana na matamanio yao. Na pia ulipohukumu kati yao kwa hukumu ya Mwenyezi Mungu yenye kuafikiana na yale waliyo nayo, hawakuridhika na hilo, bali walilipa mgongo, na pia hawakuliridhia. Amesema Yeye Mtukufu, "Na hao," ambao kitendo chao ni hivyo kwa Waumini. Yaani, hii si tabia ya Waumini, na hawafailii hata kidogo kuamini. Kwa sababu waliyafanya matamanio yao kuwa miungu wao, na wakafanya hukumu za imani kufuata matamanio yao.