Skip to content
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Ghaafir
Sūrah 40

Al-Ghaafir

This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.

Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22

Verses 45–46

فَوَقَىٰهُ ٱللَّهُ سَيِّـَٔاتِ مَا مَكَرُوا۟ ۖ وَحَاقَ بِـَٔالِ فِرْعَوْنَ سُوٓءُ ٱلْعَذَابِ 45 ٱلنَّارُ يُعْرَضُونَ عَلَيْهَا غُدُوًّا وَعَشِيًّا ۖ وَيَوْمَ تَقُومُ ٱلسَّاعَةُ أَدْخِلُوٓا۟ ءَالَ فِرْعَوْنَ أَشَدَّ ٱلْعَذَابِ 46

{45 - 46} "Basi Mwenyezi Mungu akamlinda na ubaya wa hila walizozifanya." Yaani, Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Mwingi wa kurehemu, alimlinda mwanamume huyo muumini aliyemwezesha kutokana na adhabu za yale ambayo Firauni na familia yake walimpangia ya kumwangamiza, kwa sababu alianzisha yale waliyoyachukia na akawaonyesha kwamba anaafikiana kikamilifu na Musa, amani iwe juu yake, na akawalingania katika yale ambayo Musa aliwaitia. Na hili ni jambo ambalo hawawezi kulistahimili, kwani wao ndio waliokuwa na uwezo wakati huo na alikuwa amewakasirisha, kwa hivyo wakamchukia zaidi. Basi wakataka kumfanyia vitimbi, lakini Mwenyezi Mungu akamlinda kutokana na vitimbi vyao na njama zao, na vitimbi na njama zao hizo zikawageukia wenyewe. "Na adhabu mbaya itawazunguka watu wa Firauni." Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwazamisha wote kabisa asubuhi na katika maisha ya kaburini. "Wanaonyeshwa Moto asubuhi na jioni. Na itakapofika Saa ya Kiyama patasemwa: Waingizeni watu wa Firauni katika adhabu kali kabisa!" Hizi ndizo adhabu mbaya zaidi zinazowapata wale waliokadhibisha Mitume wa Mwenyezi Mungu na wakakaidi amri yake.