An-Nisaa
This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.
Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ إِذَا ضَرَبْتُمْ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ فَتَبَيَّنُوا۟ وَلَا تَقُولُوا۟ لِمَنْ أَلْقَىٰٓ إِلَيْكُمُ ٱلسَّلَـٰمَ لَسْتَ مُؤْمِنًا تَبْتَغُونَ عَرَضَ ٱلْحَيَوٰةِ ٱلدُّنْيَا فَعِندَ ٱللَّهِ مَغَانِمُ كَثِيرَةٌ ۚ كَذَٰلِكَ كُنتُم مِّن قَبْلُ فَمَنَّ ٱللَّهُ عَلَيْكُمْ فَتَبَيَّنُوٓا۟ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرًا 94
{94} Mwenyezi Mungu Mtukufu anawaamuru waja wake Waumini wanapotoka kwenda katika jihadi katika njia yake na kutafuta radhi zake, kwamba wachunguze na wathibitishe katika mambo yao yote yenye shaka. Kwani, mambo ni ya aina mbili: yaliyo wazi, na yasiyokuwa wazi. Basi yaliyo wazi ni bainifu na hayahitaji kuthibitishwa na kufafanuliwa; kwa sababu hilo ni kutafuta lililo tayari. Na ama masuala yenye utata, yasiyokuwa wazi. Kwa hivyo, mtu anahitaji kuthibitisha katika hayo na kutafuta kubainishiwa, ili ajue je ayaendee au hapana? Kwa maana, kuthibitisha katika mambo haya kunaleta manufaa mengi na kunazuia maovu makubwa. Ambayo, kwayo inajulikana dini ya mja na akili yake na utimamu wake. Tofauti na yule ambaye anayafanyia mambo haraka katika mwanzo wake kabla ya kubainikiwa hukumu yake. Basi, hilo linafikisha kwa yale ambayo hayafai. Kama ilivyowatokea wale ambao Mwenyezi Mungu aliwalaumu katika Aya hii wakati hawakuthibitisha, na wakamuua yule aliyewasalimia, na alikuwa na kondoo wake au mali ya mtu mwingine, wakidhani kwamba anajizuia kwa hilo wasimuue. Na hili lilikuwa kosa katika jambo lenyewe. Ndiyo maana akawalaumu kwa kauli yake, “wala msimwambie anayewatolea salamu: Wewe si Muumini; kwa kutaka manufaa ya maisha ya dunia hii, hali ya kuwa kwa Mwenyezi Mungu ndiko zipo ghanima nyingi.” Yani msibebwe na mapambo yenye kuisha, machache juu ya kufanya yasiyopaswa kufanya, basi yakawakosa yale ambayo yako kwa Mwenyezi Mungu ya malipo makubwa, ya milele. Kwa kuwa yale yaliyo kwa Mwenyezi Mungu ni bora na ya kudumu zaidi. Na katika hili kuna ishara kwamba mja anatakiwa ikiwa ataona makusudio ya nafsi yake yanaelekea katika hali ambayo anatamani, ilhali ni yenye kumdhuru; kwamba aikumbushe yale ambayo Mwenyezi Mungu amemwandalia yule anayejizuia na matamanio yake, na akatanguliza radhi ya Mwenyezi Mungu mbele ya kuridhika kwake mwenyewe. Kwani, katika hilo kuna kutia moyo nafsi katika kufuata amri ya Mwenyezi Mungu, hata ikiwa hilo ni gumu kwake. Kisha Yeye Mtukufu akasema akiwakumbusha hali yao ya mwanzo kabla ya kuongoka kwao kwenye Uislamu. “Hivyo ndivyo mlivyokuwa nyinyi zamani, na Mwenyezi Mungu akawaneemesha” yani kama vile alivyowaongoa baada ya kupotea kwenu, vivyo hivyo ndivyo huwaongoa wengineo. Na kama vile uwongofu uliwafanyikia kidogo kidogo, vivyo hivyo ndivyo walivyo wengineo. Basi kuzingatia kwa aliye kamili ile hali yake ya awali iliyo pungufu, na kuamiliana kwake yule aliye katika mfano wake ile hali yake kulingana na yale anayojua katika hali yake ya awali, na kumlingania kwa hekima na mawaidha mazuri ni miongoni mwa sababu kubwa zaidi za kumnufaisha na kunufaika kwake. Ndiyo maana akairudia amri kwa kutafuta kubainishiwa, akasema, “Basi chunguza!” Na ikiwa yule aliyetoka kwenda kupigana katika njia ya Mwenyezi Mungu na kupigana vita na maadui wa Mwenyezi Mungu, na akajitayarisha kwa kila aina ya maandalizi ya kuwaumiza, anaamrishwa kuchunguza yule anayemsalimia, na ushahidi ukawa ni mkubwa kwamba alimsalimia tu kwa kuogopa kuuawa, na kwa kuihofia nafsi yake. Basi hilo linaashiria amri ya kutafuta kubainishiwa na kuthibitisha katika hali zote ambazo zina aina fulani ya mchanganyiko. Kwa hivyo anapaswa athibitishe ndani yake mpaka jambo hilo liwe wazi kwake, na libainike la uwongofu na lile la usahihi. “Hakika, Mwenyezi Mungu kwa yale mnayoyatenda anazo habari zote” na atamlipa kila mmoja yale aliyoyafanya na aliyoyakusudia kulingana yale aliyoyafanya katika hali za waja wake na makusudio yao.