An-Nisaa
This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.
Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22
وَإِنْ خِفْتُمْ أَلَّا تُقْسِطُوا۟ فِى ٱلْيَتَـٰمَىٰ فَٱنكِحُوا۟ مَا طَابَ لَكُم مِّنَ ٱلنِّسَآءِ مَثْنَىٰ وَثُلَـٰثَ وَرُبَـٰعَ ۖ فَإِنْ خِفْتُمْ أَلَّا تَعْدِلُوا۟ فَوَٰحِدَةً أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَـٰنُكُمْ ۚ ذَٰلِكَ أَدْنَىٰٓ أَلَّا تَعُولُوا۟ 3
{3} Yani, na mkiogopa kuwa hamtafanya uadilifu kwa mayatima wanawake [ambao] wako chini ya ulinzi wenu na katika ulezi wenu, na mkaogopa kuwa hamtawatekelezea haki zao kwa kuwa hamuwapendi, basi waendeeni wengineo, na muoe, "mnaowapenda katika wanawake." Yani, mliowachagua miongoni mwa wanawake wenye dini, na mali, na urembo, na heshima, na nasaba, na yasiyokuwa hayo katika sifa zinazosababisha kuwaoa. Basi chagueni kwa rai yenu. Na miongoni mwa bora zaidi kinachochaguliwa katika hayo ni sifa ya dini, kama alivyosema Nabii - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, - “Mwanamke anaolewa kwa sababu nne: kwa mali yake, na kwa urembo wake, na kwa nasaba yake, na kwa dini yake. Basi jishindie mwenye dini, mkono wako wa kulia ukajipake vumbi.” Na katika aya hii, kuna kwamba mtu anapaswa kuchagua kabla ya kufunga ndoa. Bali Mwenye Sheria alimruhusu kumtazama yule ambaye anataka kumuoa. Ili aoe baada ya kuwa na elimu juu ya jambo lake hili. Kisha akataja idadi ya wanawake aliowaruhusu, na akasema, "Wawili au watatu au wanne." Yani mwenye kupenda kuchukua wawili; na afanye, au watatu; na afanye, au wanne; na afanye, wala asiongeze juu ya hiyo. Kwa sababu, Aya hii ilitajwa ili kuonyesha neema. Kwa hivyo, hairuhusiwi kuzidisha juu ya yale aliyoyataja Mwenyezi Mungu kwa kauli moja. Na hilo ni kwa sababu mwanamume huenda matamanio yake yasiishe kwa mmoja, basi akaruhusiwa mmoja baada ya mwingine mpaka wafike wanne. Kwa sababu, katika wanne kuna kutoshelezwa kwa kila mtu isipokuwa katika hali adimu. Na pamoja na haya, yeye anaruhusiwa kufanya hivyo ikiwa nafsi yake itakuwa salama kutokana na dhuluma, na akajiamini katika kuwatekelezea haki zao. Lakini akiogopa kitu katika jambo hili, basi na aachie kwa mmoja au yule ambaye mkono wake wa kulia unamiliki. Kwa sababu, si wajibu kwake kugawanya kwa usawa katika wanawake ambao mkono wake wa kulia unamiliki. "Hilo," yani, kumwoa mmoja tu au yule ambaye mkono wake wa kulia unamiliki, "ndilo karibu zaidi kwamba msiegemee;" yani, kudhulumu. Na katika hili kuna kwamba mja hapaswi kuliendea jambo ambalo anahofiwa kufanya dhuluma na kutotekeleza wajibu hata ikiwa linaruhusika. Bali inalazimu awe na wasaa na kuwa salama. Kwa maana, kuwa salama ndicho kitu bora zaidi anachoweza mja kupewa.