Skip to content
Tafsir As-Saadi - Swahili · An-Nisaa
Sūrah 4

An-Nisaa

This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.

Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22

Verse 23

حُرِّمَتْ عَلَيْكُمْ أُمَّهَـٰتُكُمْ وَبَنَاتُكُمْ وَأَخَوَٰتُكُمْ وَعَمَّـٰتُكُمْ وَخَـٰلَـٰتُكُمْ وَبَنَاتُ ٱلْأَخِ وَبَنَاتُ ٱلْأُخْتِ وَأُمَّهَـٰتُكُمُ ٱلَّـٰتِىٓ أَرْضَعْنَكُمْ وَأَخَوَٰتُكُم مِّنَ ٱلرَّضَـٰعَةِ وَأُمَّهَـٰتُ نِسَآئِكُمْ وَرَبَـٰٓئِبُكُمُ ٱلَّـٰتِى فِى حُجُورِكُم مِّن نِّسَآئِكُمُ ٱلَّـٰتِى دَخَلْتُم بِهِنَّ فَإِن لَّمْ تَكُونُوا۟ دَخَلْتُم بِهِنَّ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ وَحَلَـٰٓئِلُ أَبْنَآئِكُمُ ٱلَّذِينَ مِنْ أَصْلَـٰبِكُمْ وَأَن تَجْمَعُوا۟ بَيْنَ ٱلْأُخْتَيْنِ إِلَّا مَا قَدْ سَلَفَ ۗ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ غَفُورًا رَّحِيمًا 23

Aya hizi tukufu zinajumuisha wanawake walioharamishwa kwa sababu ya nasaba, na walioharamishwa kwa sababu ya kunyonya, na walioharamishwa kwa sababu ya ndoa na walioharamishwa kwa sababu ya kuunganisha; na wale walio halali miongoni mwa wanawake.

{23} Basi kuhusu wale walioharamishwa kwa sababu ya nasaba, wao ni saba ambao Mwenyezi Mungu aliwataja: Mama: Na anaingia ndani yake kila ambaye ni sababu ya kuzaliwa kwako, hata kama ni wa mbali. Na anaingia katika binti kila mmoja ambaye wewe ndiye sababu ya kuzaliwa kwake. Na madada wa kwa baba na mama au wa kwa baba au wa kwa mama. Na shangazi, ambaye ni kila dada wa baba yako au babu yako, hata kama watapanda juu vipi. Na halati, ambaye ni kila dada wa mama yako au nyanya wako hata kama atapanda juu vipi, awe mrithi au la. Na binti za kaka, na binti za dada, hata kama watashuka chini vipi. Basi hawa ndio walioharamishwa katika nasaba, kwa mujibu wa makubaliano ya wanachuoni, kama yalivyo maandishi ya Aya tukufu. Na wasiokuwa wao, wanaingia katika kauli yake, "Na mmehalilishiwa wasio kuwa hao." Nao ni kama binti ya shangazi, na wa ami, na binti wa mjomba na wa halati. Na ama kuhusu wale walioharamishwa kwa sababu ya kunyonya, hao Mwenyezi Mungu alitaja miongoni mwao mama na dada. Na katika hilo kuna kumharamisha mama pamoja na kwamba maziwa si yake, bali ni ya (mwanamume) mwenye maziwa. Na hili linaashiria kwa tanabahisho yake kwamba mwenye maziwa ni baba wa yule aliyenyonyeshwa. Na ikiwa uzazi wa baba na uzazi wa mama utathibiti, basi kitathibiti kile ambacho ni tawi lao, kama vile undugu wao na ubabu na unyanya wao, na vizazi vyao. Na Nabii - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-alisema, "Ni haramu kwa sababu ya kunyonyesha kile ambacho ni haramu kwa sababu ya nasaba." Kwa hivyo uharamu linaenea katika upande mama aliyenyonyesha na yule ambaye, maziwa ni yake kama unavyoenea katika jamaa na mtoto aliyenyonyeshwa kwa dhuria yake peke yake. Lakini kwa sharti ya kwamba kunyonya kuwe mara tano katika ule umri wa miaka miwili kama Sunnah ilivyoonyesha. Na ama wale walioharamishwa kwa sababu ya ndoa, hao ni wanne: wake wa baba, hata kama (baba hao) watapanda juu vipi. Na wake wa watoto, hata kama (watoto hao) watashuka chini vipi, wawe warithi au wawe waliozuiwa kurithi. Na mama za mke, hata kama (mama hao) watapanda juu vipi. Hawa watatu wanakuwa haramu kwa kufunga mkataba tu. Na wanne ni binti wa kambo. Naye ni binti wa mkewe, hata kama watashuka chini vipi. Na huyu hawi haramu mpaka amwingilie mkewe (ambaye ndiye mama yake binti huyu). Kama alivyosema hapa, "na watoto wenu wa kambo walio katika ulinzi wenu waliozaliwa na wake zenu mliowaingilia," hadi mwisho wa Aya. Na wengi wa wanachuoni walisema: Kauli yake, "walio katika ulinzi wenu," ni kufungilia kulikotumiwa kwa sababu hilo huwa hivyo mara nyingi na wala hakuna maana isiyokuwa ya moja kwa moja. Kwa maana, binti wa kambo ni haramu hata kama hayuko katika ulinzi wake. Lakini kufungia hivi kuna faida mbili: moja yake ni kwamba [ndani yake] kuna tanabahisho juu ya hekima katika kuharamisha binti wa kambo, na kwamba yeye yuko katika nafasi ya binti. Nayo pili ni kwamba ndani yake kuna ushahidi wa kuruhusika kuwa faragha na binti wa kambo, na kwamba yuko katika nafasi sawa na wale ambao yuko katika ulinzi wake miongoni mwa mabinti zake na mfano wao. Na Mwenyezi Mungu ndiye anayejua zaidi. Na ama wale walioharamishwa kwa sababu ya kuwaoa kwa pamoja, hao Mwenyezi Mungu alitaja kuwaowa dada wawili kwa pamoja na akaharamisha hilo. Na Nabii - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - aliharamisha kuoa kwa pamoja mwanamke na shangazi yake, au halati yake. Kwani ni haramu kila wanawake wawili ambao kati yao kuna tumbo la uzazi. Na lau kuwa itakadiriwa kwamba mmoja wao ni wa kiume na mwingine ni wa kike, basi anakuwa haramu juu yake, kwa kuwa ni haramu kuwaoa kwa pamoja. Kwa sababu ya yale yaliyo katika hilo ya sababu za kukatana kati ya watu wa tumbo moja.