An-Nisaa
This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.
Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22
إِن تُبْدُوا۟ خَيْرًا أَوْ تُخْفُوهُ أَوْ تَعْفُوا۟ عَن سُوٓءٍ فَإِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَفُوًّا قَدِيرًا 149
{149} Kisha Yeye Mtukufu akasema, "Mkidhihirisha wema au mkiuficha," Na hili linajumuisha kila heri, ya kimaneno na ya kimatendo, ya dhahiri na iliyofichika, sawa iwe wajibu au inayopendekezwa. "Au mkiyasamehe mabaya, yaani, kutoka kwa yule anayewafanyia mabaya katika miili yenu, na mali zenu, na heshima zenu, basi msameheeni; kwani, malipo ni ya aina sawa na matendo. Kwa hivyo mwenye kusamehe kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu atamsamehe. Na mwenye kufanya wema, mwenyezi Mungu atamfanyia wema. Ndiyo maana akasema, "basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, Muweza." Yaani, Anasamehe makosa ya waja Wake na madhambi yao makubwa, hivyo Anawatandazia pazia lake, kisha Anaamiliana nao kwa msamaha Wake kamili unaotokana na uwezo Wake. Na katika Aya hii kuna mwongozo wa kufahamu maana ya majina ya Mwenyezi Mungu na sifa zake, na kwamba uumbaji na amri vinatokana na hayo, na yanataka hivyo. Na ndiyo maana anatoa sababu ya hukumu mbalimbali kwa majina mazuri sana kama katika Aya hii, alipotaja kufanya wema na kumsamehe aliyefanya ubaya. Akafungamanisha hilo na kutuelekeza katika kuyajua majina yake, na kwamba hilo linatutosheleza kutaja malipo yake maalum.