Az-Zumar
This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.
Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22
إِنَّآ أَنزَلْنَآ إِلَيْكَ ٱلْكِتَـٰبَ بِٱلْحَقِّ فَٱعْبُدِ ٱللَّهَ مُخْلِصًا لَّهُ ٱلدِّينَ 2
{2} Lakini pamoja na hayo, kitabu hiki kiliongeza kuwa wazi katika ukamilifu wake kwa sababu ya yule aliyeteremshiwa, yaani Muhammad - rehema na amani zimshukie - ambaye ndiye mtukufu zaidi katika viumbe vyote, kwa hivyo ikajulikana kuwa ndicho kitabu kitukufu zaidi. Na pia kiliongeza kuwa wazi kwa sababu ya yale ambayo kiliteremka nayo, ambayo ni Haki. Kiliteremka na haki isiyo na shaka yoyote ndani yake, ili kuvitoa viumbe katika giza mbalimbali na kuvipeleka kwenye nuru. Na kilishuka kikiwa na haki katika habari zake za ukweli na hukumu za uadilifu. Kwa hivyo kila kitu ambacho kitabu hiki kinaashiria ndiyo aina kuu zaidi ya haki inayohusiana na mambo yote ya kielimu yanayotakiwa. Basi hakuna chochote kilicho baada ya haki isipokuwa upotofu. Na kwa vile kiliteremka kutoka kwenye haki huku kimejumuisha haki, kikiwa kimeteremka kwa mtukufu zaidi katika viumbe vyote ili kuviongoa viumbe; kikawa kina neema kubwa na kikatukuka. Na ikawa ni lazima kushukuru neema hii kwa kumkusudia Mwenyezi Mungu peke yake katika dini. Ndiyo maana akasema: "Basi muabudu Mwenyezi Mungu ukimsafia Dini Yeye tu," miongoni mwa sheria za dhahiri na sheria zilizofichika: Uislamu, imani na ihsan, kwa kumpwekesha Mwenyezi Mungu pekee kwa hayo na kuutaka uso wake kwa hayo pasi na kukusudia lengo lingine lolote.