Skip to content
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Qasas
Sūrah 28

Al-Qasas

This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.

Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22

Verse 3

نَتْلُوا۟ عَلَيْكَ مِن نَّبَإِ مُوسَىٰ وَفِرْعَوْنَ بِٱلْحَقِّ لِقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ 3

{3} Miongoni mwa mambo ambayo iliyabainisha ni kisa cha Musa na Firauni; alikitaja na kukirudia katika maeneo kadhaa, na akakieleza kwa kina mahali hapa. Alisema "Tunakusomea katika habari za Musa na Firauni kwa Haki" kwa maana habari zao ni za ajabu, "kwa ajili ya watu wanaoamini." Kwani hao ndio wanaoongeleshwa, kwa kuwa wana imani na ndio wanayatafakari, na kuyakubali, na kuongoka kutoka kwa mahali penye mazingatio, na wanazidi imani kwa hayo na yakini na heri pamoja na heri yao. Na ama wengineo, hao hawafaidiki kitu kwa hayo isipokuwa kuwasimamishia hoja tu, na Mwenyezi Mungu aliilinda dhidi yao, na akaweka kati yake na wao pazia wasiifahamu.