Skip to content
Tafsir As-Saadi - Swahili · Ash-Shu'araa
Sūrah 26

Ash-Shu'araa

This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.

Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22

Verses 119–122

فَأَنجَيْنَـٰهُ وَمَن مَّعَهُۥ فِى ٱلْفُلْكِ ٱلْمَشْحُونِ 119 ثُمَّ أَغْرَقْنَا بَعْدُ ٱلْبَاقِينَ 120 إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَةً ۖ وَمَا كَانَ أَكْثَرُهُم مُّؤْمِنِينَ 121 وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ ٱلْعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ 122

{119-122} "Kwa hivyo tukamwokoa yeye na waliokuwa pamoja naye katika marikebu iliyosheheni," watu na wanyama. "Kisha tukawazamisha baadaye;" yaani, baada ya Nuhu na wale waliokuwa pamoja naye miongoni mwa waumini "waliobakia" wote katika kaumu yake. "Hakika katika hayo" ya kumuokoa Nuhu na wafuasi wake na kuwaangamiza wale waliomkadhibisha, "ipo ishara" inayoashiria ukweli wa Mtume wetu na usahihi wa kile walicholeta na ubatili wa kile walichofanyiwa na maadui zao waliokanusha. "Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Yeye Mwenye nguvu," aliyeshinda maadui kwa nguvu zake kwa kuwaangamiza kwa mafuriko. "Mwingi wa kurehemu" vipenzi wake ambapo alimuokoa Nuhu na wale waliokuwa pamoja naye katika watu wa imani.