Skip to content
Tafsir As-Saadi - Swahili · Ash-Shu'araa
Sūrah 26

Ash-Shu'araa

This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.

Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22

Verses 1–2

طسٓمٓ 1 تِلْكَ ءَايَـٰتُ ٱلْكِتَـٰبِ ٱلْمُبِينِ 2

{1 - 2} Yeye Muumba Mtukufu anaashiria ishara inayoonyesha kuzitukuza aya za Kitabu kinachobainisha, kilicho wazi ambacho kinaonyesha matashi yote ya kimungu na makusudio yote ya kisheria, kwa njia ya kwamba haibakii kwa mwenye kuzitazama shaka yoyote wala fikira potofu katika yale aliyojulisha au katika yale aliyohukumu, kwa sababu ya uwazi wake na kuashiria kwake maana tukufu zaidi na hukumu mbalimbali kuhusiana na hukumu yake. Na Mtume wa Mwenyezi Mungu - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - alikuwa akiwaonya watu kwacho, na anaongoza kwacho njia iliyonyooka, kwa hivyo wakaongoka kwa hilo waja wa Mwenyezi Mungu wachamungu, na anazipa mgongo aliyeandikiwa kuwa mashakani. Kwa hivyo akawa anahuzunika huzuni mkubwa juu ya kutoamini kwao; kwa sababu ya kuwatakia heri na kuwashauri.