Al-Furqaan
This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.
Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22
وَقَالَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ لَوْلَا نُزِّلَ عَلَيْهِ ٱلْقُرْءَانُ جُمْلَةً وَٰحِدَةً ۚ كَذَٰلِكَ لِنُثَبِّتَ بِهِۦ فُؤَادَكَ ۖ وَرَتَّلْنَـٰهُ تَرْتِيلًا 32
{32} Haya ni miongoni mwa mapendekezo ya makafiri ambayo nafsi zao zinawapendekezea, wakasema, "Kwa nini hakuteremshiwa Qur-ani yote mara moja tu?" Kama vilivyoteremshwa vitabu vya kabla yake. Na ni kitu gani kilichokatazwa kiko katika kushuka kwake kwa njia hii? Bali kuteremka kwake kwa njia hii ndiyo kamilifu na bora zaidi. Na ndiyo sababu akasema, "Hayo ni hivyo," tuliiteremsha sehemu sehemu "ili tuuimarishe kwayo moyo wako." Kwa sababu, kila kinapomteremkia kitu katika Qur-ani, anazidi kuwa na utulivu na kuwa imara, haswa wakati kuna sababu ya kumtia wasiwasi. Kwa hivyo kuteremka kwa Qur-ani wakati wa kutokea kwake kunakuwa na sehemu kubwa na kuimarisha kwingi kuliko ikiwa ingeteremka kabla ya hayo, kisha akamkumbuka tu wakati sababu zake zinapotokea. "Na ndiyo tumeisoma kwa mafungu." Yaani, tulifanya muhula katika kuiteremsha na kukupeleka hatua hatua. Yote haya yanaonyesha kuwa Mwenyezi Mungu anakijali na kukitunza Kitabu chake cha Qur-ani na Mtume wake Muhammad, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, kwa kuwa alifanya kuteremka kwa Kitabu chake hiki kufanyike kulingana na hali za Mtume na masilahi yake ya kidini.