Al-Muminoon
This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.
Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22
وَإِنَّكَ لَتَدْعُوهُمْ إِلَىٰ صِرَٰطٍ مُّسْتَقِيمٍ 73 وَإِنَّ ٱلَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِٱلْـَٔاخِرَةِ عَنِ ٱلصِّرَٰطِ لَنَـٰكِبُونَ 74
{73-74} Katika aya hizi tukufu, Mwenyezi Mungu alitaja kila sababu inayopatisha imani, akataja vizuizi, na akabainisha yanayofisadi imani moja baada ya nyingine, na akataja katika vizuizi, kwamba mioyo yao iko katika hofu, na kwamba hawakuzingatia neno, na kwamba waliwafuata baba zao, na kwamba walisema: Mjumbe wao ana wazimu; kama yalivyotangulia maelezo yao. Na alitaja Mola miongoni mwa mambo ya muhimu katika imani yao: Ni kuizingatia Qur-ani, na kupokea neema za Mwenyezi Mungu kwa kuzikubali, na ufahamu wa hali ya Mtume Muhammad- rehema na amani za Mwenyezi Mungu iwe juu yake, - na ukamilifu wa ukweli wake na uaminifu wake, na kwamba yeye hawaombi ujira kwa hayo, na kwamba hakika vitendo vyake ni kwa ajili ya manufaa yao na maslahi yao, na kwamba hayo anayowalingania juu yake ndiyo njia nyoofu, iliyo sahali kwa wafanyao kwa unyoofu wake, inayowasilisha kwa makusudio kwa ukaribu zaidi, iliyo safi na nyepesi; iliyo safi katika tauhidi, nyepesi katika kuitenda; ulinganizi wako kwao katika njia iliyonyooka ni wajibu kwa anayetaka haki kukufuata; kwa sababu ni katika yale yanayoshuhudika kwa akili na maumbile kwa uzuri wake na kuwafikika kwake kwa maslahi; basi wanaenda wapi wasipokufuata wewe? Hakika wao hawana yatayowatajirisha na kuwatosheleza dhidi ya kukufuata wewe Mtume, kwa kuwa wao "katika njia." Wamejitenga, wamejiepusha, wamepotoka katika njia inayofikisha kwa Mwenyezi Mungu na katika nyumba ya karama zake. Hawana katika mikono yao ila upotefu na ujinga, na hivi hivi ndivyo alivyo kila aliyekhalifu haki. Hapana budi ila atakuwa mpotefu katika mambo yake yote. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu, "Na ikiwa hawakuitikii, basi jua kuwa wanafuata pumbao lao tu. Na nani aliyepotea zaidi kumshinda anayefuata pumbao lake bila ya uwongofu utokao kwa Mwenyezi Mungu."