Skip to content
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Muminoon
Sūrah 23

Al-Muminoon

This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.

Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22

Verse 70

أَمْ يَقُولُونَ بِهِۦ جِنَّةٌۢ ۚ بَلْ جَآءَهُم بِٱلْحَقِّ وَأَكْثَرُهُمْ لِلْحَقِّ كَـٰرِهُونَ 70

{70} "Au wanasema, ana wazimu?" Yaani: wazimu; ndiyo maana alisema aliyosema! Na mwendawazimu hasikilizwi, na maneno yake hayana funzo, kwa sababu anaropoka uongo na maneno ya kejeli! Katika kuwajibu, Mwenyezi Mungu alisema katika maneno haya, "Bali amewajia kwa Haki;" yaani, kwa amri thabiti ambayo ni ukweli na uadilifu , ambayo haina tofauti wala utata; basi itakuwaje kwamba, aliyekuja nayo ana wazimu? Inaweza tu kuwa katika kiwango cha juu cha ukamilifu kutokana na elimu, akili na maadili mazuri! Na vile vile; katika hii kuna mwendelezo wa yale yaliyotangulia. Yaani, uhakika uliowazuia wao kuamini ni kwamba, "Amewajia kwa Haki,na wengi wao wanaichukia Haki." Na Haki kubwa zaidi aliowajia nayo ni: Ikhlasi kwa kumuabudu Mola pekee, na kuacha walioabudu dhidi ya Mwenyezi Mungu, na hakika alijua chuki yao juu ya jambo hili na kustaajabia kwao kwalo; na kuwa kwake Mtume alikuja kwa Haki, na kuwa kwao ni wachukivu kwa Haki kwa asili, ndilo lililowawajibishia kukanusha Haki; siyo kwamba walikuwa na shaka wala kuwakanusha Mitume. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu, "Basi hakika wao hawakukanushi wewe, lakini hao madhalimu wanazikataa Ishara za Mwenyezi Mungu.