Skip to content
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Anbiyaa
Sūrah 21

Al-Anbiyaa

This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.

Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22

Verse 10

لَقَدْ أَنزَلْنَآ إِلَيْكُمْ كِتَـٰبًا فِيهِ ذِكْرُكُمْ ۖ أَفَلَا تَعْقِلُونَ 10

{10} Yaani, "Hakika tumewateremshia" enyi mliotumiwa Muhammad bin Abdullah bin Abdul-Muttalib "Kitabu" kitukufu na Qur-ani iliyo wazi "ambacho ndani yake kuna ukumbusho wenu." Yaani, utukufu wenu, fahari yenu na kunyanyuka kwenu (cheo). Ikiwa mtakumbuka kwacho yale yaliyomo miongoni mwa habari za ukweli, na mkaziitakidi, na mkatekeleza amri zilizo ndani yake, na mkaepuka makatazo yaliyo ndani yake, basi kitanyanyuka cheo chenu na jambo lenu litakuwa kubwa. "Je, hamtumii akili" kuhusu yale yenye kuwanufaisha na yenye kuwadhuru? Vipi hamfanyii kazi yale yenye ukumbusho wenu na utukufu wenu katika dunia na akhera? Na lau kama mngalikuwa na akili, mngaliifuata njia hii. Na pindi hamkuifuata na mkafuata njia isiyokua hii miongoni mwa njia mbalimbali ambazo ni zenye kuwapoteza na kuwafanya wadhalilifu katika dunia na akhera, na kuwa kwenu mashakani humo, ikajulikana kuwa hamna akili iliyo sahihi au maoni yaliyo sawa. Na aya hii inasadikishwa na yale yaliyotokea. Kwa maana, wanaomuamini Mtume na wale waliokumbuka kutokamana na Qur-ani miongoni mwa maswahaba na wale waliowafuata baada yao, walipata kunyanyuliwa daraja na utukufu wa ajabu, na cheo cha kikubwa na heshima juu ya wafalme, jambo ambalo kila mmoja analijua, na tena inajulikana vyema yale yaliyowatokea wale ambao hawakuinyanyulia kichwa Qur-ani hii, wala hawakuongoka kwayo na kutakasika kwayo ya chuki, udhalili, kuharibikiwa mambo, na kuwa mashakani. Kwa hivyo, hakuna njia yoyote ya kufikia furaha ya duniani na Akhera isipokuwa kwa kukumbuka kwa Kitabu hiki.