Taa-Haa
This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.
Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22
طه 1 مَآ أَنزَلْنَا عَلَيْكَ ٱلْقُرْءَانَ لِتَشْقَىٰٓ 2
{1 - 2} Neno "Taha" ni miongoni mwa herufi za mkato zilizofunguliwa kwazo sura nyingi, na si jina la Nabii - rehema na amani za Mwenyezi ziwe juu yake. "Hatukukuteremshia Qur-ani ili upate mashaka." Yaani, makusudio yetu katika ufunuo na kukuteremshia Qur-ani juu yako na kukuwekea sheria si ili upate mashaka kwa hayo, na tena si kuweka katika sheria majukumu yenye uzito juu ya waliojukumishwa kisheria, na watendaji wakashindwa nguvu ya kuyatenda. Lakini Ufunuo, Qur-an, na sheria aliviweka hivyo Yeye Mwingi wa kurehemu, Mwingi wa Rehema, na akavifanya viwe ni vya kufikisha katika furaha, kufanikiwa na kufaulu, na akavifanya kuwa rahisi zaidi. Na akarahisisha njia zake na milango yake yote, na akavifanya kuwa chakula cha mioyo na roho, na mapumziko kwa miili. Kwa hivyo, maumbile ya asili yaliyo salama, na akili nyoofu zikavipokea kwa kuvikubali na kutii, kwa kuwa zilijua kwamba vina heri ndani yake katika dunia na Akhera.