Taa-Haa
This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.
Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22
فَلَا يَصُدَّنَّكَ عَنْهَا مَن لَّا يُؤْمِنُ بِهَا وَٱتَّبَعَ هَوَىٰهُ فَتَرْدَىٰ 16
{16} Yaani, asikuzuie na kukushughulisha kutoiamini Saa (ya Qiyama) na malipo na kuifanyia hiyo matendo yeyote ambaye aliikufuru, asiyeitakidi kutokea kwake, anayefanya bidii kuitilia shaka na kuwafanya wengine kuishuku, na anaijadili kwa batili, na anasimamisha fikira potovu awezavyo kuhusiana nayo, anayefuata matamanio yake kuhusiana nayo. Basi jihadhari na kumsikiliza ambaye hii ndiyo hali yake au hata kukubali chochote katika maneno yake, matendo yake yenye kumzuia mtu kuiamini na kuifanyia bidii inavyopasa. Na Mwenyezi Mungu alitahadharisha juu ya mtu ambaye hii ndiyo hali yake, kwa sababu ndiyo ya kuhofisha zaidi juu ya muumini kwa sababu ya wasiwasi ambayo yanamtia, kumdanganya, na kwa sababu nafsi zimeumbwa huku zinapenda kujifananisha na kuiga wana aina yake. Na katika hili kuna tanabahisho na ishara juu ya kujihadharisha na kila mwenye kuita kwenye batili, anayezuia kuwa na imani ya wajibu au kuikamilisha imani hiyo, au mwenye kutia fikira potofu katika moyo, na kujitahadharisha na kuangalia vitabu vyenye hayo. Alitaja katika hii kumuamini, kumuabudu na kuiamini Siku ya Mwisho, kwa sababu mambo haya matatu ndiyo misingi ya imani na nguzo ya dini. Na yakitimia, inatimia suala la dini. Na upungufu wake au hata kupotea kwake ni kwa sababu ya upungufu wa haya au kupunguka kitu kwayo. Na hili ni mfano wa kauli yake Yeye Mtukufu katika kujulisha kuhusu mizani ya furaha ya makundi ambayo yalipewa Kitabu na kuwa kwayo mashakani, "Hakika wale walioamini, na Mayahudi na Masabii na Wakristo, mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu, na Siku ya Mwisho, na akatenda mema, basi hawatakuwa na hofu yoyote wala hawatahuzunika." Na kauli yake, "ukaja kuangamia'" ikiwa utafuata njia ya mwenye kuizuia. Na kauli yake Yeye Mtukufu: