Al-Baqara
This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.
Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22
قُلْ مَن كَانَ عَدُوًّا لِّجِبْرِيلَ فَإِنَّهُۥ نَزَّلَهُۥ عَلَىٰ قَلْبِكَ بِإِذْنِ ٱللَّهِ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ وَهُدًى وَبُشْرَىٰ لِلْمُؤْمِنِينَ 97 مَن كَانَ عَدُوًّا لِّلَّهِ وَمَلَـٰٓئِكَتِهِۦ وَرُسُلِهِۦ وَجِبْرِيلَ وَمِيكَىٰلَ فَإِنَّ ٱللَّهَ عَدُوٌّ لِّلْكَـٰفِرِينَ 98
(97-98) Yani waambie hawa Mayahudi ambao walidai kuwa kilichowazuia kuamini ni kwamba rafiki yako ni Jibril amani iwe juu yake, na lau kuwa angelikuwa asiyekuwa yeye miongoni mwa Malaika wa Mwenyezi Mungu, basi wangekuamini na kukusadiki. Hakika, madai yenu haya ni mgongano haya ni yenye kupingana, na kuanguka chini, kumfanyia Mwenyezi Mungu kiburi. Kwani Jibril, amani iwe juu yake, ndiye aliyeiteremsha Qur-ani kutoka kwa Mwenyezi Mungu ndani ya moyo wako. Naye ndiye aliyeteremsha kwa Manabii wa kabla yako, na Mwenyezi Mungu ndiye aliyemuamrisha na kumtuma na hayo. Basi, yeye ni Mtume tu, pamoja na kwamba kitabu hiki alichoteremka nacho Jibril kinasadikisha vilivyokitangulia miongoni mwa vitabu bila ya kutofautiana navyo wala kuvipinga. Na ndani yake mna uwongofu mkamilifu kutokana na kila aina ya upotovu, na bishara ya heri ya kidunia na kiakhera kwa mwenye kuiamini. Basi uadui juu ya Jibril anayeelezwa kwa hayo ni kumkufuru Mwenyezi Mungu na Aya zake, na uadui kwa Mwenyezi Mungu na Mitume wake na Malaika wake. Kwa maana, uadui wao juu ya Jibril sio kwa ajili yake mwenyewe, bali ni kwa sababu ya haki aliyoteremka nayo kutoka kwa Mwenyezi Mungu juu ya Mitume wa Mwenyezi Mungu. Basi inajumuisha kufuru na uadui kwa yule aliyeiteremsha na kuituma, na yule ambaye alitumwa nayo, na yule aliyetumiwa. Na hii ndiyo sababu ya hilo.